DADA POA WAFIKISHANA MAHAKAMA WAKIGOMBANIA BWANA

0

 Mnamo Ijumaa, Disemba 9,2022 kahaba alifikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kumpiga kitutu mwenzake, mbele ya Hakimu Mkuu wa Mombasa.Mariam Issa Mohammed aliyefika mbele ya Hakimu Mkuu Vincent Adet alikiri shtaka la kumpiga na kumjeruhi mwenzake Anita Mtengo.

Mahakama iliachwa kinywa wazi baada ya Mariam kusimulia peupe chanzo cha ugomvi hadi kupigana kwa mangumi na mateke. 

Alisema kuwa yeye ni kahaba na mwathiriwa ni mwenzake wanaofanya kazi hiyo katika Soko la Sega, eneo la Majengo Mombasa.
ULITAZAMA VIDEO HII YA KUPATA PESA MTANDAONI

Kulingana na Mariam, walitofautiana na mwenzake baada ya kushusha bei ya huduma kutoka bei ya kawaida ya KSh 350 (sawa na takribani shilingi shilingi 6000 ya Tanzania) hadi KSh 150 sawa na shilingi 3000 ya Tanzania)  na hivyo basi kumharibia biashara.

 Tukio hilo lilifanyika mnamo Jumatano, Disemba 7, kwa mujibu wa maelezo ya kesi hiyo. 

Wawili hao walikatizwa mara kwa mara na hakimu wakati walipoanza kubishana na kurushina maneno machafu ambayo hawapaswi kutamka ndani ya kortini.


Mtengo aliiomba mahakama kumshurutisha mshatkiwa alipe gharama zote za matibabu, baada ya kumpiga kitutu na kumjeruhi. 

"Nimeumia sana na mkono wangu umejeruhiwa. Ninataka nilipwe fidia ya KSh 40,000 niliyotumia kwa matibabu," Mtengo alisema.

Chanzo - Tuko News
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top