Akisoma hukumu hiyo katika shauri la madai namba 4 la mwaka 2021,hakimu mkazi JOVITH KATO alisema mahakama imepitia ushahidi wa pande zote mbili na kujiridhisha kwamba KOMANYA KITWALA alitenda kosa hilo Januari 5 mwaka 2020 na hivyo mahakama imemuhukumu kulipa kiasi hicho cha fedha Milion 80 badala ya shilingi Milion 140 ambazo mlalamikaji ALEXANDER NTONGE alizodai kulipwa kutokana na makosa ya udhalilishaji aliyofanyiwa na KOMANYA KITWALA wakati alipokuwa mkuu wa wilaya ya Tabora mjini.
Awali wakili wa mlalamikaji KELVIN KAYAGA aliiambia mahakama KOMANYA KITWALA alikwenda nyumbani kwa mlalamikaji akiwa na askari Polisi ambao aliwaamuru kumkamata na kumtesa kisha kumuweka ndani katika Kituo Kikubwa cha Polisi Tabora mjini bila kuwa na kosa lolote ambapo baadae aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora kwa wakati huo ACP SAFIA JONGO aliagiza mlalamikaji ALEXANDER NTONGE kuachiliwa huru kwa madai kulikuwa hakuna kosa lolote lililofanya kukamatwa na kuwekwa ndani jambo ambalo lilionekana ni udhalilishaji wa waziwazi uliokuwa umefanywa na kiongozi huyo wa Serikali ya wilaya kwa wakati huo.
Chanzo - Tabora Press Club