Jeshi la polisi Mkoani Mtwara linamshikilia mwanamke mkazi wa Kijiji cha Sinde Kata ya Msangamkuu, halmashauri ya Mtwara, kwa tuhuma za kumnyonga mtoto wake mwenye umri wa miaka miwili na nusu
Baadhi ya majirani wanasema mama huyo alimnyonga mtoto wake huku yeye na mtoto wakiwa utupu (bila nguo) na kukimbilia porini ndipo majirani walipomkimbiza na kumchukua mtoto lakini alikuwa tayari amefariki
Kaimu Kamanda jeshi la polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Nicodemus Katembo amesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani pindi uchunguzi utakapokamilika.
USISAHAU HII VIDEO NI MUHIMU UWEZE KUITAZAMA