ISHU YA FEISAL YAZUA GUMZO,TAMKO YANGA LATOLEWA

0

 Hatimaye Mchezaji Feisal Salum amewaaga rasmi Mashabiki wa Yanga na kuthibitisha kweli kwamba anaondoka kwenye Club hiyo na kusisitiza kuwa atayakumbuka yote mazuri akiwa Yanga na kuyasahau yote mabaya kwa haraka sana.


Taarifa ya Feisal aliyoiweka mtandaoni inasomeka kama ifuatavyo "Umekuwa wakati mzuri kuichezea Club ya Young Africans yenye historia kubwa na ya kuvutia nchini na Afrika yote, tumekuwa na nyakati nyingi mchanganyiko, tulifurahi pamoja pale furaha ilipokuja uelekeo wetu na tulihuzunika pamoja nyakati mbaya zilipotutokea"

"Nitakumbuka mengi mazuri yaliyotutokea pamoja na nitasahau yoye mabaya kwa haraka sana, kila nikikumbuka Mashabiki wa WANANCHI moyo unakuwa mzito kuwaaga hivyohivyo kwa Wachezaji wenzangu na Viongozi pia kwa upendo mliouonesha tukiwa pamoja kwenye shida na raha lakini lisilo budi hutendwa au hunenwa kwahiyo leo nasema KWAHERINI WANANCHI"

"Maisha ndivyo yalivyo, mambo huja na kupita na kuna wakati yanajirudia, mpaka wakati mwingine tena kwaherini ya kuonana"

BAADA YA MASAA KADHAA CLUB YA YANGA IKATOA TAARIFA HII

KLABU ya Yanga inapenda kuujulisha umma na Wanachama wa Yanga kuhusiana na taarifa za mchezaji wetu Feisal Salum Abdallah zinazoenea katika mitandao ya kijamii.

Klabu inathibitisha kupokea barua kutoka kwa mchezaji tarehe 23 Disemba 2022 inayoeleza kuvunja Mkataba wake baina yake na Klabu.

Klabu ya Yanga imemuandikia na kumjibu Feisal na miongoni mwa majibu ni kama ifuatavyo;

Hakuna misingi ya kikanuni wala kisheria kulingana na mkataba wake ambazo zinampa haki mchezaji kusitisha mkataba wake na Klabu kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba wa sasa Kanuni na Taratibu za FIFA ziko wazi na zimeelezea taratibu zote juu ya Jambo la aina hii.

Kwamba, Mkataba baina ya mchezaji na Klabu hauwezi kuvunjwa na upande mmoja tu bila kujadiliana na upande wa pili wakati msimu wa ligi ukiwa unaendelea.

Kwamba, kwa mazingira hayo, barua ya mchezaji ina dhana potofu na haina misingi ya kisheria ya kuvunja mkataba baina ya klabu na mchezaji Na kwa mantiki hiyo, tumemuagiza Feisal, azingatie matakwa ya mkataba wake kama ilivyoelezwa katika mkataba huo.

Klabu pia imemkumbusha Feisal, mkataba wake wa sasa ni halali hadi ifikapo Tarehe 30 Mei 2024 Pamoja na hayo, tunapenda kuujulisha umma kuwa, kwa kuthamini kiwango na mchango wa Faisal kwa klabu yetu, tayari tulishaanza mazunguzo baina ya klabu ya Yanga na wawakilishi wa Feisal wakiongozwa na mama mzazi wa mchezaji ili kuboresha maslahi yake na kuongeza muda wa mkataba wake wa sasa ambao unaishia Mei 2024.

Hata hivo, Klabu haijapokea majibu mbadala wa mapendekezo ya maboresho haya kutoka upande wa Feisal na wawakilishi wake na badala yake tumepokea barua inayoelezea kuvunja mkataba kutoka upande wa Feisal ambayo ni Kinyume na makubaliano ya mkataba wake wa sasa.

Klabu tayari imesharejesha fedha kiasi cha TZS 112,000,000 (Millioni Mia Moja na Kumi na mbili) ambazo Feisal aliziweka katika Akaunti za Klabu.

Tunapenda kueleza kuwa, kuna taratibu na kanuni za Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) na zile za Shirikisho la Mpira wa miguu Duniani (FIFA) ambazo ni lazima zifuatwe na timu yoyote ile inayotaka kumsajli mchezaji yeyote wa Klabu ya Young Africans SC (YANGA).

Yanga, inasisitiza kuwa, Feisal Salum Abdallah ni mchezaji halali ya Yanga na ana mkataba hadi kufikia Mei 30, 2024.

Imetolewa na Idara ya Habari
Young Africans Sports Club.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top