JAMAA ANASWA AKIWAFUNDISHA WATOTO USHOGA GEITA

0

 

Jabir Hamisi, mkazi wa mtaa wa Mwatulole, mkoani Geita, amenusurika kuuawa kwa kipigo na mamia ya wananchi, baada ya kukutwa akiwa na kundi la watoto wadogo, akiwafundisha vitendo vya ushoga na ulawiti, hali iliyolazimu Jeshi la Polisi mkoani humo kuingilia kati na kumuondoa katika eneo hilo, ili kunusuru maisha yake.

Akizungumza mara baada ya kukamatwa na wananchi Jabir amesema kitu kilikuwa kinasababisha akiona makundi ya watoto anawaonesha sehemu zake za siri na kuanza kuzichezea, ni kwa sababu tangu afike Geita hajawahi kufanyiwa kitendo hicho ndio maana akajikuta anatumia njia mbalimbali ili aweze kupata watu wa kumfanyia hivyo.


Baadhi ya wananchi waliokuwepo eneo la tukio wamesema kijana huyo alikuwa akifika kwenye makundi ya watoto alikuwa anatoa sehemu zake za siri na kuanza kuzichezea huku akiwahamasisha watoto hao nao wafanye hivyo.


Mwenyekiti wa Polisi jamii Mtaa huo Itanga Timoth amesema walivyomuhoji mtuhumiwa huyo amekiri kwamba yeye ni shoga na vitendo hivyo alivianzia jijini Dar Es Salaam huku mwenyekiti wa mtaa huo Noel Ngasa akiwataka wazazi kuwa walinzi wa kwanza wa watoto wao ili kuwaepusha na vitendo vinavyochochea uharibifu wa maadili.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top