"JUKUMU LA KUPAMBANA NA RUSHWA SIO LA 'ZAECA' PEKEE, BALI NI JUKUMU LA WANANCHI WOTE" KAIMU KAMANDA WA ZAECA KUSINI PEMBA.

Hassan Msellem
0

Waandishi wa habari wametakiwa kuwa mabalozi wazuri katika kutoa elimu kwa wananchi juu ya mapambano dhidi ya rushwa na uhujumu uchumi ili kuhakikisha wananchi wanashiriki katika mapambano hayo.


Akisoma hotuba huko katika Uwanja wa Gombani Pemba,, katika shamra za kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku kupambana na rushwa duniani yanayotarajiwa kufanyika tarehe 16, mwezi huu, Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Mheshimiwa Abdalla Rashid Ali, ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika matembezi hayo, amesema vyombo vya habari ni muhimili muhimu katika mapambano dhidi ya rushwa, hivyo waandishi wa habari wana jukumu kubwa la kuhakikisha wananchi wanafikwa na elimu hiyo.


"Matembezi haya yamelenga kuyakumbusha Makundi mbali mbali katika Jamii kuwa chachu ya kuhimiza uadilifu, uwajibikaji na kukataa vitendo vya rushwa hapa nchini" alisema


"Jumuiya ya Kimataifa imekuwa ikiadhimisha siku ya mapambano dhidi ya rushwa tarehe 09 December kila mwaka,  Zanzibar ikiwa ni miongoni mwa nchi inayoamini katika falsafa ya uwazi, uwajibikaji na utawa Bora, imekuwa ikiungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha siku hii" Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Mhe. Abdalla Rashid Ali


Nae, Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Mheshimiwa Khatib Juma Mjaja, Serikali zote mbili za Tanzania zimeanzisha vyombo vya kupambana na rushwa na uhujumu uchumi ambavyo ni ZAECA Kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na TAKUKURU kwa Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuhakikisha fedha za Serikali zinatumika ipaswavyo.


Kwa upande wake, kaimu Kamanda wa ZAECA Mkoa wa Kusini Pemba Ndugu. Mustafa Hassan Issa, amesema jukumu la kupambana na rushwa sio la taasisi ya ZAECA pekee, bali ni jukumu la kila mwananchi katika kuhakikisha wananchi wanapata haki zao kwa mujibu wa Sheria.


Mwakilishi wa Gombani Fitness Center, ameiomba viongozi wa taasi ya kuzuia rushwa na uhujumu uchumi Zanzibar (ZAECA) kutokujiingiza katika vitendo vya rushwa na uhujumu uchumi, kwani kufanya hivyo kutaondosha Imani ya uadilifu kwa taasisi hiyo Kwa wananchi.


"Niwaombe sana, kujiepusha na vitendo vya rushwa na uhujumu uchumi, kwani mutakapojiingiza katika vitendo hivyo wananchi watapoteza imani ya uadilifu kwenu na badala ya vitendo vya rushwa na uhujumu uchumi mutashindwa kuvidhibiti ipaswavyo" alisema


Maadhimisho ya siku ya kupambana na rushwa duniani yanatarajiwa kufanyika tarahe 16 mwezi huu, ambapo kwa mwaka huu maadhimisho hayo yatafinyika katika Ukumbi wa Idriss Abdul Wakili Kikwajuni, huku kauli mbiu ya "MKATABA WA UMOJA WA MATAIFA DHIDI YA RUSHWA UNAUNGANISHA DUNIA KUPAMBANA NA RUSHWA"

Kikundi Cha Gombani Fitness Center, kikifanya mazoezi katika Uwanja wa Gombani Pemba, ikiwa ni shamra shamra za kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya mapambano dhidi ya rushwa duniani December 16 kwa upande wa Zanzibar.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top