Pia ameagiza ndani ya kipindi cha miezi mitatu wapeleke maji kwa wananchi wakati huo matenki ya maji yakiendelea kujengwa huku akisisitiza mradi huo kujengwa kwa kasi ili maji yawafikie wananchi ipasavyo
Katibu Mkuu ametoa maagizo hayo mwishoni mwa wiki alipofanya ziara ya kukagua mradi wa maji Isapulano ambao pia uanatarajiwa kuongeza maji Makete mjini ambapo Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji Makete mjini Alphonce Kahimba ametoa taarifa ya ujenzi wa mradi huo kwa kusema tarayi ujenzi wa chanzo cha maji na ulazaji wa bomba umbali wa kilomita 4.9 umekamilika huku ikitarajiwa kujenga matenki mawili ya ukubwa wa cubic mita 200
Ndipo Katibu Mkuu Mhandisi Sanga akatoa maagizo ya ujenzi wa tenki la lita laki 5 badala ya laki 2 na kuahidi kuwaongezea na wataalamu kutoka maeneo mengine ili washirikiane kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa kasi na ukamilike mapema ili wananchi wapate maji kwa kuwa kwa jiografia ya Makete haitakiwi wapate maji kwa asilimia 80 bali wapate maji kwa asilimia 100
Amewahimiza kujenga mradi huo kwa kasi hivyo kuahidi kuwaongezea wataalamu kutoka maeneo mengine ikiwemo Mbeya ili wasaidiane na maeneo mengi ikiwemo ya Makete mjini yapate maji kwani hakuna sababu ya wananchi kulalamika maji Makete
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Isapulano Alphonce Mbilinyi amesema vipi vitongoji viwili katika kijiji cha Isapulano wananchi wake wanalazimika kuchota maji mtoni kwa kuwa huduma ya maji ya bomba bado haijawafikia hivyo kwa maelekezo ya katibu mkuu anaimani tatizo hilo litakwisha
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Makete Clemence Ngajilo amesisitiza umuhimu wa wataalamu hao kusimamia utakelezaji wa mradi huo ili ukamilike kwa wakati huku mkuu wa wilaya ya makete Juma Sweda akisisitiza wananchi kutunza miundombinu ya maji.