MADIWANI WATISHIA KUMTIMUA MWANASHERIA WA HALMASHAURI

0

 Madiwani wa halmashauri ya wilaya Biharamulo mkoani Kagera wametishia kuazimia na kuwafukuza mwanasheria wa halmashauri hiyo pamoja na afisa kilimo kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yao na kupelekea wakulima wa Tumbaku wilayani humo kudhurumiwa kiasi cha shilingi milioni 50.


Katika baraza la madiwani la robo ya kwanza lililofanyika mwishoni mwa wiki hii, Diwani wa kata ya Kalenge Eriki alitaka kupata majibu juu ya hatua iliyofikiwa ya kulipwa kwa wakulima wa tumbaku waliokopwa tumbaku yao na kampuni ya Jaspen ambayo ilichukua tumbaku ya wakuima takribani miaka miwili sasa.

Akijibu hoja hiyo afisa kilimo wa halmashauri hiyo Brono Ngawagala alilieleza baraza hillo kuwa kwa mujibu wa mkataba Amkosi iliyoingia mkataba na kampuni ya Jaspen inatakiwa kwanza kabla kushitaki mahakamani ipeleke shauri hilo kwenye bodi ya tumbaku kwaajili ya usuluhishi na hivi ndivyo hali ilivyokuwa.

BOFYA KUTAZAMA VIDEO HII,ITAKUSAIDIA LEO
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top