Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza imesema Washtakiwa 81 kati ya 84 akiwemo Diana Bundala maarufu Zumaridi katika kesi namba 12 ya kufanya kusanyiko lisilohalali na shambulio la kudhuru mwili hawana kesi ya kujibu.
Hakimu Mkazi Mwandamizi Clescensia Mushi akisoma uamuzi huo amesema pasina shaka Mahakama imejiridhisha kwamba Washtakiwa walioachiwa huru katika kesi namba 12 hawakuguswa na vipengele muhimu vinavyotakiwa kuthibitisha makosa ya jinai.
Washtakiwa watatu kati ya 84 ndio wamekutwa na kesi ya kujibu kwa mujibu wa sheria ambao ni Juma Khamis mshtakiwa namba 05, Meshack Joseph namba 33 pamoja Daud Manyanda namba 45, ambapo Hakimu Mkazi Mwandamizi Clescensia Mushi akaihairisha kesi hiyo na itatajwa tena December 20, 2022 kwa Washtakiwa Watatu
Hata hivyo Diana Bundala maarufu Zumardi bado anakabiliwa na kesi mbili ambazo ni kesi namba 10 Shambulio la kuzuia Maafisa wa Serikali kutekeleza majukumu yao na kesi namba 11 ya usafirishaji haramu wa Binadamu.
USIKOSE KUTAZAMA VIDEO HII YA FURSA ZA MTANDAONI