MAKETE ACHENI KUFUMBIA MACHO VITENDO VYA UKATILI-APOLLO

0

 

Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya wiki ya huduma ya msaada wa Kisheria Apollo Laizer ambaye pia ni Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Makete.

Na Edwin Moshi, MAKETE

Wananchi wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kutoyafumbia macho matukio ya ukatili yanayojitokeza katika maeneo yao kwani kwa kufanya hivyo kwa kuwa zipo sheria zinazosimamia masuala hayo ili zifuatwe na haki itendeke

 

Hayo yamebainika leo Desemba 5, 2022 katika ufunguzi wa wiki ya msaada wa kisheria tukio lililofanyika kiwilaya katika kijiji cha Kisinga kata ya Lupalilo wilayani hapo kabla ya kufikia kilele chake Desemba 10, 2022

 

Akizungumza kwenye ufunguzi huo, Mkurugenzi wa shirika la wasaidizi wa Kisheria wilaya ya Makete (MAPAO) Mch. Denis Sinene amesema ni wakati sasa wa jamii ya Makete kuacha kukaa kimya na badala yake waripoti pale wanapoona vitendo vya ukatili vinapofanyika ili hatua ziweze kuchukuliwa

"Tujitokeze kutoa taarifa, vyombo saivi vipo salama, uongozi wa vijiji vyenu upo,uongozi wa kata upo, nenda katoe taarifa, na nyie watoto tumewaita hapa ukiona mtu anasema neno lisilofaa kamwambie mama, kamawambie baba, nenda kamwambie kiongozi kwamba huyu nimeona ananishikashika sehemu ambazo sitaki, sasa unakaona na kenyewe kanasema shika sana halafu na lizee lenyewe, mmesikia nyie vijana wangu hapo" amesema Mkurugenzi Sinene

 

Amesema watu wanafanya matukio sio kwamba hayapo Makete, matukio yapo lakini watu wanaficha uovu hivyo kijiji cha Kisinga kinatakiwa kubadilika na kuwa mfano wa vijiji vingine vyote vya wilaya ya Makete


Kwa upande wake Mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya Makete Apollo Laizer ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa maandimisho hayo amesema matukio yote ya ukatili yanayotokea katika jamii yaripotiwe kwenye vyombo husika ikiwemo kwa jeshi la polisi kwa kuwa ukatili unapofanyika hautakiwi kufichwa ndani ya jamii kwa madai ya kusuluhishwa

"Hata viongozi wa serikali ya kijiji msifichefiche masuala ya ukatili yanayojitokeza na kujaribu kuyasuluhisha, hapana, yapelekwe mahala husika ili haki itendeke kwa waathirika, matatizo mengine ya ukatili yanayojitokeza yanapelekea msongo wa mawazo hata mara nyingine watu wengine kujitoa uhai, lakini wanapopata haki wanapopata msaada wa kisheria msongo wa mawazo utaondoka na wataweza kurudi katika jamii, lakini pia wale wanaotekeleza vitendo vya ukatili ni lazima waadhibiwe kwa mujibu wa sheria" amesema Laizer

 

Amesema vitendo vingi vya ukatili wa kijinsia vinavyofanyika katika jamii ni vitendo vya jinai hivyo sio vitendo vya kusema watu wanakaa mezani na kuyamaliza hivyo vinatakiwa kupelekwa katika vyombo husika ikiwemo kuvitolea taarifa polisi katika dawati la jinsia na ikibidi vipelekwe mahakamani ili mwisho wa siku kuwe na jamii inayozingatia utawala wa kisheria

 

Aloyce Msigwa, Lucida Salum na Mwl. Zuhura Mussa ni wakazi wa kijiji cha Kisinga ambapo wameieleza Edmo Blog kuwa elimu ya masuala ya usaidizi wa kisheria ifike kwenye kila kijiji kwa kuwa kumekuwa na vitendo vya ukatili vinavyotokea lakini haviripotiwi na vinafanywa kuwa siri, hivyo kushauri vinapojitokeza ni vema vikaripotiwa ili haki itendeke.
BOFYA VIDEO HII KUTAZAMA FURSA ZA MTANDAONI
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top