MATUKIO 1000 YA UTELEKEZAJI WATOTO YARIPOTIWA MBEYA

0

Ukatili dhidi ya watoto umeendelea kushika Kasi Mkoani Mbeya na maeneo mbalimbali ya hapa Nchini, wakati Dunia ikifikia kilele Cha maadhimisho ya siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia, Mkoa wa Mbeya yameripotiwa matukio 1074 ya utelekezaji wa watoto.

Wimbi hili la utelekeza wa watoto limechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la matukio ya ubakaji na ulawiti kwa watoto wa kiume Mkoani humo, ambapo matukio 226 ya ubakaji na ulawiti Kwa watoto yameripotiwa Kwa kipindi cha mwaka huu.

Kutokana na matukio haya watoto wengi wamekua wakiangukia kupata malezi katika vituo vya kulelea watoto na baadhi yao wakiangukia kua watoto wa mtaani kutokana na kukosa malezi bora ya Mama na Baba baada ya kutelekezwa kama anavyo tueleza Jason Fihavangu Mkurugenzi wa kituo Cha kulelea watoto Cha Nuru kilichopo Uyole Jijini Mbeya.

Kutokana na vituo hivi kijitoa katika malezi ya watoto hawa, wananchi, vikundi mbalimbali na taasisi wamekua ndio faraja kubwa kwao pale wanapoungana katika kutoa huduma za chakuka na mavazi, kama walivyo fanya kikundi Cha Wanawake Cha Vision Woman na baadhi ya Wananchi kutoka Kata ya Ilomba hapa Jijini Mbeya.

Katika kilele Cha siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mbeya Stella Kategile ameeleza namna ambavyo Mkoa umekua ukifanya jitihada za kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.

BOFYA HAPA CHINI KUTAZAMA VIDEO HII

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top