MBOWE ASEMA 'INAUDHI KUAMBIWA NIMELAMBA ASALI'

0

 Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe wakati akiongea na Diaspora nchini Marekani leo amesema anakasirishwa na wanaosema amelamba asali ili kumfanya akae kimya, na kusema hilo ni kama tusi kwake lakini anavumulia kwakuwa ni sehemu ya harakati.

Freeman Mbowe

“Nimekuwa nikifuatilia mijadala katika mitandao, hisia za Viongozi wenzangu ndani ya Chama, hisia za Watanzania wengine wasio Wana CHADEMA, wengi wakiamini kwamba maridhiano (Kati ya CHADEMA na Serikali) ni kupoteza muda, na hapo katikati ukatokea msamiati kuwa Mbowe kalamba asali, mbona Mbowe hazungumzi, Mbowe amekuwa kimya sana”

“Naomba leo niweke rekodi sawa, Chama ninachokiongoza nimekiruhusu sana kusema wala sitaki kiwe Chama ambacho akizungumza Mwenyekiti basi wenzake wote wakae kimya, hapana”

“Kwanza katoka Makamu wangu Lissu akazungumza, ukimsikia Lissu kasema ukiangalia kwa haraka unaweza kufikiria Mbowe na Lissu wana ugomvi lakini huyu ni Mtu amepigwa risasi 16 hawa ni Viongozi wenzangu wamefungwa Jela, wanaishi ughaibuni kwa kulazimishwa, ni lazima uelewe hisia na uchungu wao, hii ya ‘Mbowe kalamba asali’ inaniudhi lakini inabidi nikubali, nikasema OK, kama kulamba asali ni kuitetea Nchi yangu niko tayari kuitetea”

TAZAMA VIDEO HII

“Nimekuwa kwenye upinzani kwa miaka 30, sio kwa kuangalia madaraka wala fedha bali mustakabali wa Tanzania, nimepoteza vitu vingi, hiyo asali nitakayopewa leo inaweza kufidia miaka yangu 30 ya jasho na maumivu?, ni tusi lakini tunaikubali kwasababu ni sehemu ya harakati”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top