MBUNGE ASEMA MSILALAMIKIE JUU YA TOZO,IMEOKOA WANANCHI WETU

0

 

Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Anne Kilango Malecela amesema kupitia fedha zitokanazo na tozo serikali chini ya rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miezi 20 amepewa shilingi Bil.3 ambapo katika fedha hizo shillingi Bil 1.5 imetokana na fedha za Tozo.


Mbunge huyo amesema wananchi wasilalamike juu ya tozo hizo kwani imeokoa wananchi wengi kupitia miundombinu ya barabara kwani wananchi wengi walikua wanashindwa kwenda maeneo kadhaa kutokana na ubovu wa barabara lakini kwa sasa katika jimbo hilo kila barabara ina mkandarasi na kazi inaendelea.

Amesema TARURA wanaendelea na kazi usiku na mchana na kumuomba mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu kupelekea shukrani za wananchi wa jimbo hilo kwa rais Samia Suluhu Hassan kwani ametatua kero ya barabara iliyodumu kwa miaka yote.

TAZAMA VIDEO HII KWA UNDANI ZAIDI
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top