MBUNGE WA JIMBO LA CHAMBANI, ATOA MSAADA WA SARUJI KWA MISIKITI YA CHUMBAGENI NA WAMBAA.

Hassan Msellem
0
Mbunge wa Jimbo la Chambani Mheshimiwa Mohammed Abrahman Mwinyi, ametoa msaada wa mifuko thelathini (30) ya saruji Kwa misikiti miwili (2) ya Shehia ya chumbageni na Wambaa, ambayo waumini wa misikiti hiyo walitoa ombi kwa Mbunge huyo ili kuendeleza harakati zao za Ujenzi wa nyumba hizo za ibada.


Akikabidhi msaada huo kwa waumini wa Shehia ya chumbageni na Wambaa, Diwani wa wadi ya Ndugu. Ngwachani Mohammed Said Ali, amesema kutolewa kwa msaada huo ni juhudi za viongozi wa Jimbo la Chambani katika kuhakikisha wanachangia katika shughuli mbali mbali na Dini na kijamii.


"Tupo hapa Kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo letu la Chambani Mheshimiwa Mohammed Abrahman Mwinyi, ambaye mulifikisha maombi yenu kwake naye akaahidi kuyafanyia kazi, sasa leo tupo hapa kukamilisha ahadi hiyo na hii inadhihirisha wazi kuwa viongozi wetu wapo Kwa ajili ya wananchi wote wa Jimbo hili bila ya kuzingatia itikadi ya dini wala chama katika kuwaletea wananchi maendeleo" alisema 

Akipokea msaada huo wa mifuko ishirini (20) ya saruji Kwa niaba ya waumini wa msikitini wa chumbageni, Mwenyekiti wa tawi la chumbani Ndugu. Juma Shaaban Jabir, amesema wanawashukuru viongozi wa Jimbo hilo Kwa moyo wao wa kuwasaidia wananchi wa Jimbo hilo bila ya kujali itikadi zao za Dini wala vyama vya siasa, jambo ambalo linajenga Imani njema kwa Wananchi wa Jimbo hilo.
Mwenyekiti wa tawi la chumbani Ndugu. Juma Shaaban Jabir, akimshukuru Mbunge wa Jimbo la Chambani kutokana na msaada huo wa mifuko ishirini ya saruji katika ujenzi wa msikiti wa chumbageni.


Kwa upande wake Imamu msaidizi msikiti wa Wambaa Mohammed Suleiman Khelef, amesema msaada huo wa mifuko kumi (10) utasaidia katika kuendeleza harakati za ujenzi katika Msikiti huo.
Msaidizi msikiti wa Wambaa Mohammed Suleiman Khelef, akitoa neno la shukurani baada ya kupokea msaada huo.

"Kwa niaba ya waumini wote wa msikiti huu, hatuna budi kuwashukuru Sana viongozi wa Jimbo la Chambani hususan Mheshimiwa Mbunge Kwa moyo wake wa dhati wa kuweza kutusaidia mifuku hii kumi ya saruji ambayo itatusaidia Kwa kiasi kikubwa katika ujenzi wa jengo letu hili, ni Imani yetu kuwa hata tutakapohitaji msaada mwengine ataweza kutusaidia kwa moyo mkunjufu nasi tuseme kuwa tunamshukuru sana na tunamtakia kila lenye kheri katika maisha yake ya uongozi na baada ya uongozi" 

Msaada huo wa mifuko thelathini (30) ya saruji imetolewa katika misikiti miwili ya chumbageni na Wambaa, ambapo Kwa upande wa msikiti wa chumbani wamesaidiwa mifuko 20 na Wambaa mifuko 10, ikiwa ni msaada wa Mbunge wa Jimbo la Chambani Mheshimiwa Mohammed Abrahman Mwinyi.


Jimbo la Chambani liko katika Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, likiwa ni Jimbo kubwa zaidi kati ya majimbo nne (4) ya Wilaya ya Mkoani ambayo ni Chambani yenyewe, Mkoani, Kiwani na Mtambile.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top