MCH NG'ANG'A AWAONYA WANAUME WANAOWAPIGIA MAGOTI WAKE ZAO

0

 Mhubiri James Ng'ang'a maarufu kama Pasta Ng'ang'a amewashauri wanaume jinsi ya kuishi vizuri na wake zao lakini kupiga magoti si moja ya nasaha zake.


Ng'ang'a amewaonya wanaume dhidi ya kuwapigia magoti wanawake wanapoomba msamaha akisema hicho ni kitendo cha uoga ambayo haifai kuwa sifa ya mwanaume.

Kwa mujibu wa mhubiri huyo, watu hukoseana katika ndoa na wanaume wanapaswa kutumia mbinu mbadala kuomba wake zao msamaha badala ya kuwapigia magoti. "Wanaume msiwe mnapiga magoti kwa wanawake hata ukimkosea. Sisi huwa hatupigi magoti kwa wanawake, tunamnunulia kakitu," Pasta Ng'ang'a alisema.

Mchungaji huyo wa kanisa la Neno Evangelism Centre anasema kuwa ni wanawake ndio wanaostahili kuwapigia waume zao magoti na wala si vinginevyo.
  "Yeye ndio anafaa apige magoti, akuambie samahani. Sisi hatupigi magoti, sisi ndio makomando. Ukitaka mke wako aone umetubu, unamnunulia kitu," Pasta Ng'ang'a aliongeza.
Chanzo: Tuko
BOFYA HAPA KUTAZAMA VIDEO HII
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top