MCHUNGAJI ATUHUMIWA KUMNAJISI MTOTO WA MIAKA 13

0

 

Jeshi la Polisi nchini Zambia, linamsaka Mchungaji wa Kikongo anayejulikana kwa jina la Mike Mapalo anayedaiwa kumnajisi mtoto wa miaka 13 .


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Copperbelt, Peacewell Mweemba amesema tukio hilo lilitokea Desemba 17, 2022 katika kitongoji cha Ndola kilichopo mjini Lubuto, majira ya saa 22:00 usiku.

Amesema, mtoto huyo mwathiriwa anatoka eneo la Luapula kuja Ndola kwa ajili ya likizo kumtembelea shangazi yake na alikumbwa na mkasa huo baada ya kunajisiwa hali iliyopelekea kupata maumivu sehemu za siri.

Kamanda Mweemba amefafanua kuwa, “Siku hiyo ya maafa, shangazi yake hakuwepo nyumbani na msichana alikuwa amebaki na mshukiwa ambaye ni mpenzi wa shangazi yake na alitumia nafasi hiyo kukamilisha unyama alioutenda.” 

Aidha, inaarifiwa kuwa baada ya kitendo hicho, mtuhumiwa alikimbia na mwathiriwa alikwenda kumjulisha shangazi yake mwingine ambaye alitoa taarifa Polisi huko Lubuto huku taarifa zikionesha kuwa mshukiwa huyo amekimbilia nchini kwake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top