MKE ACHOMWA NA MAJI YA MOTO NA MDENI WA MUMEWE

0

 Cecilia Kingi Muuo wa Likoni, Kaunti ya Mombasa ameshtakiwa kwa kumjeruhi vibaya Faith Chelang'at baada ya kumchoma na maji moto na kumuacha na majeraha mabaya.

Muuo alifikishwa kortini siku ya Alhamisi, Disemba 22,2022 mbele ya Hakimu Mkuu wa Mombasa Vincent Adet na kukana mashtaka dhidi yake.

Kwa mujibu wa maelezo ya kesi, mnamo Jumatatu, Disemba 19, katika mtaa wa Jamvi la Wageni, Likoni, Chelang'at alikwenda kwa nyumba ya mshtakiwa na kutaka kujua iwapo mumewe alikuwa nyumbani. Chelang'at alimfahamisha Muuo kuwa mumewe alikuwa na deni lake la KSh 200 alizohitaji kununua chakula cha jioni.


Muuo ndipo akamfahamisha Chelang'at, kwamba mumewe hayuko ila anaweza kumsubiri arejee huku akirejea jikoni kupika sima.

 Muda mchache Muuo alirejea na maji moto na kumchoma Chelangat ambaye sasa anatibiwa katika Hospitali ya Coast General. 

Mayowe ya mwathiriwa yaliwavutia majirani waliompeleka hospitalini. 

"Mheshimiwa mimi sina hatia. Huo ni uwongo, na simjui mwanamke huyo, wala sijawahi kumuona. Pengine amepagawa. Ninaweza vipi kumchoma mtu ambaye sijawahi kumuona na bila sababu..." Cecilia alijibu wakati aliposomewa mashtaka.


Mshtakiwa aliachiliwa kwa bondi ya KSh 50,000 na mdhamini sawa. Kesi hiyo imeratibiwa kutajwa mnamo Januari 11, 2023 kabla ya huku kutolewa. 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top