Waandishi wa habari Kisiwani Pemba wameombwa kuzitumia vyema kalamu zao ili kuandika habari zenye kuleta maslahi mapana kwa taifa.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti mstaafu wa Klabu ya waandishi wa habari Pemba Bwana Said
Mohammed Ali, wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa klabu hiyo huko katika Ukumbi wa maktaba Chake Chake, amesema taaluma ya habari ni taaluma muhimu sana katika ustawi wa jamii na taifa, hivyo basi waandishi wa habari wanapaswa kuitumia taaluma hiyo ili kuhakikisha Taifa linapata maslahi bora kupitia taaluma hiyo
Aidha mwenyekiti huyo mstaafu, amewaomba waandishi hao kuzingatia kanuni na misingi ya taaluma ya habari ili kuepukana na migogoro pamoja na khitilafu zinaweza kujitokeza.
"Niwaombe kuzitumia vizuri kalamu zetu, na kuzitumia vizuri kalamu zetu ni kufuatia maadili ya Uandishi wa Habari, Jamii inatutegemea Nchi inatutegemea Dunia inatutegemea musijione kwamba wewe uko hapa Pemba habari utakayoandika itaishia Pemba tu hapana bali punde tu baada ya kuchapisha Habari hiyo hususan kwenye hii mitandao ya kijamii habari punde tu inaweza kuenea dunia mzima, hivyo basi nawasihi sana kuwa Makini katika kuzingatia sheria, kanuni na maadili ya Uandishi wa Habari ili tuweze kuepukana na migogoro na khitilafu zinaweza kujitokeza" alisema
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa klabu hiyo Ndg. Bakari Mussa Juma, akiwasilisha mwelekeo wa Muungano wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) alisema wafadhili wanaofadhili klabu za waandishi wa habari nchini wamezitaka klabu hizo kuwa na mabadiliko chanya ili ziweze kujisimamia zenyewe.
Sambamba na hayo amewaomba waandishi kuitumia ipaswavyo mitandao ya kijamii ya klabu hiyo katika kuchapisha habari ili kutokana na idadi kubwa ya wafadhili na wadau wa habari ni watumiaji wa mitandao hiyo.
"Wanalolitaka wafadhili Sasa hivi ni kuwa na mabadiliko chanya ndani ya klabu zetu kwamba zinatakiwa kuwa active na zifanye shughuli zake Kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha klabu za habari nchini zinajitegemea"
Akiwasilisha mwelekeo wa klabu ya waandishi wa habari Pemba Katibu wa Klabu hiyo Ali Mbarouk Omar, amewataka wanachama wa klabu hiyo kujiongeza kitaaluma ili waweze kuandika habari zenye ubora zaidi kwa maslahi ya taifa.
Naye Msaidizi Katibu wa 'PPC' Mchanga Haroub Shehe, akiwasilisha Ripoti fupi ya Mwaka 2022, ya waandishi wa habari Pemba, amesema PPC iliyoombwa na imetekeleza mradi wa kuelimisha Jamii juu ya kifua kifua kikuu, mradi wa kushajihisha wa uwanaharakati wa kijamii ingawa mradi huo hakupatikana.
Kwa upande wa mafunzo, amesema wanachama wa PPC, walipata Mafunzo Kwa waandishi wa habari juu ya kuelimisha Jamii juu ya maradhi ya kifua kikuu kupitia wizara ya afya kitengo cha shirikishi kifua kikuu, Ukimwi na Ukoma kupitia ufadhili wa Global Fund, Mafunzo ya kujenga uwezo juu ya kutambua vipaumbele vya masuala ya kiafya katika Jamii wafadhili wakiwa ni Wizara ya afya ustawi wa jamii, Wazee, jinsia na Watoto Zanzibar, kujenga uwezo juu ya kuandaa mpango mkakati wa Mtandao wa Zanzibar Child Right Forum kutoka Shirika la Save the Children, Mafunzo juu ya utatuzi wa migogoro kupitia Shirika la Search For Common Ground, Mafunzo ya waalimu juu ya suala ya usalama Kwa waandishi wa habari ambayo yalitolewa na Muungano wa klabu za Waandishi wa habari Tanzania 'UTPC' kushiriki mafunzo na mkutano wa kimataifa wa mpango wa mafunzo kwa waandishi wa habari ITP3, kujifunza mbinu za kidumisha Amani mchango wa vyombo vya habari na malezi na makuzi ya vijana wafadhili wakiwa ni Shirika la Search For Common Ground, mkutano wa wadau Mkoa wa Kusini Pemba katika mradi wa dumisha Amani Zanzibar wafadhili wakiwa ni Foundation For Civil Society Kwa kushirikiana na Search For Common Ground, Mafunzo ya ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari na mafunzo ya awamu ya pili kwa waratibu kuhusu ufuatiliaji wa ukiukwaji wa haki za kupata taarifa, mafunzo ya Ulinzi na Usalama Kwa waandishi ya wafadhili wakiwa ni UTPC, Mafunzo ya ushawishi na utetezi wafadhili wakiwa ni PART.
"PPC kutoka mwaka 2021 hadi 2022 imefanikiwa kuongeza wanachama sita ambao ni Hassan Hamza Msellem, Juma Suleiman Haji, Khalfan Khatib Khalfan, Hanifa Salim Mohammed, Thurea Ali Mohammed, Fatma Hamad pamoja na Juma Seif Haji" alisema
Akitaja wanachama ambao walipata tuzo mbali mbali katika kazi walizozifanya kupitia tuzo za EJAT, ni pamoja Zuhura Juma Said kutoka Gazeti la Zanzibar Leo, Habiba Zarali Rukuni Gazeti la Zanzibar Leo, Haji Nassor Mohammed Zanzibar Leo, Amina Mohammed.
Katika mkutano huo, waandishi wa habari wamepatiwa vikoti maalum kutoka Muungano wa klabu za Waandishi wa Habari Tanzania 'UTPC' watakavyovitumia katika shughuli zao za Kila siku za kihabari.
Mkutano huo uliyojumuisha wanachama 53 kutoka klabu ya waandishi wa habari Pemba, umejadili muelekeo na maazimio ya mkutano mkuu wa Muungano wa klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC).
