MPENZI ABAKWA NA WAHUNI WATATU WALIOJIFANYA POLISI MPENZI WAKE AKISHUHUDIA KILA KITU

0

 Kenya wanachunguza kisa ambapo mwanamke mwenye umri wa miaka 27 alishambuliwa na kubakwa na wanaume watatu waliokuwa wamejifanya maafisa wa polisi.


Kisa hicho kilitokea kwenye njia ya giza kutoka eneo la Kiwanja kuelekea Kahawa Magharibi mnamo Jumatatu, Desemba 12, usiku.

Mwanamke huyo aliwaambia polisi kuwa alikuwa pamoja na mpenzi wake na walikuwa wakielekea nyumbani walipokabiliwa na wanaume watatu.

Wawili hao walikuwa wamenunua chakula katika kituo kimoja cha maduka na walikuwa wakielekea nyumbani walipokabiliwa na wanaume waliodai kuwa walikuwa maafisa wa polisi.

Waliwaamuru wawili hao kulala chini katika uwanja wazi wakati watatu hao walipoanza kumbaka mwanamke huyo huku mpenzi wake akitazama bila la kufanya lolote kwa kuwa watu hao walikuwa wamejihami kwa silaha ikiwemo visu.

Baada ya kukamilisha uhalifu huo wa kingono watuhumiwa hao walitoroka na kuwaacha wapenzi hao eneo hilo kisha mpenzi wake alipelekwa hospitali na hatimaye kupewa ruhusa kurejea nyumbani

Mkuu wa polisi wa Kiambu Perminus Kioi alisema bado hawajajua nia ya shambulio hilo na kwamba wanachunguza nia hiyo kwa nia ya kuwapata wabakaji.
NAKUSISITIZA TENA TAZAMA VIDEO HII

Kesi za ubakaji zimekuwa zikiongezeka nchini Kenya.

Kwa mfano, kesi za ubakaji ziliongezeka hadi 973 mwaka 2020 ikilinganishwa na 950 zilizoripotiwa mwaka 2019, 921 mwaka 2018, 784 mwaka 2017 na 923 mwaka 2016.

Kesi za unajisi ziliongezeka hadi 6,801 mwaka 2020 kutoka 5,397 mwaka 2019, 4,767 mwaka 2018, 3,487 mwaka 2017 na 4,512 mwaka 2016.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top