MTOTO AJINYONGA SABABU MBUZI KAFA

0

 Polisi katika Kaunti Ndogo ya Rachuonyo Kaskazini Mashariki, Kaunti ya Homa Bay nchini Kenya wameanzisha uchunguzi kuhusu kifo cha mwanafunzi wa darasa la saba ambaye anashukiwa kujiua

Mvulana huyo mwenye umri wa miaka kumi na miwili aliyetambulika kama Felix Odhiambo Okech alidaiwa kujitoa uhai msituni mbali na nyumbani kwao Jumamosi jioni kwa kujinyonga kwa kamba kutoka juu ya mti.

Mwanafunzi huyo wa Shule ya Msingi ya Dudi anaripotiwa kuondoka nyumbani kwenda kuwafungua mbuzi wao kutoka eneo la malisho lakini alitoweka hadi majira ya jioni ambapo mwili wake ulipatikana ukining’inia juu ya mti.

Kulingana na babake mtoto huyo Michael Okech, huenda Felix alijinyonga baada ya kupata mbuzi mmoja amekufa katika eneo la malisho chini ya hali isiyoeleweka.

Alisema kutokana na hofu hiyo, kijana huyo alitoa kamba kwenye mbuzi aliyekufa na kuitumia kujinyonga.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Rachuonyo Mashariki Justus Kucha ambaye alithibitisha kisa hicho alisema kuwa polisi hawajabaini sababu iliyomfanya mtoto huyo aamue kujitoa uhai.

Polisi sasa wameanzisha uchunguzi kuhusu kisa hicho na mwili wa mvulana huyo ulihamishwa hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya kaunti ndogo ya Rachuonyo South kwa uchunguzi wa maiti.
HII NDIO ILE VIDEO YA KUTENGENEZA PESA MTANDAONI
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top