MTOTO AJIUA KWA KUTONUNULIWA NGUO ZA SIKUKUU YA KRISMASI

0

 

Mvulana mmoja wa miaka 11 amejiua katika kijiji cha Kibongoti, kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya sababu kuu ikiwa babu na nyanyake kuchelewa kumnunulia nguo mpya za sikukuu ya Krismasi.


Akithibitisha kisa hicho, mkuu wa polisi eneo hilo Moses Koskei alisema kuwa uchunguzi katika kifo cha mwanafunzi huyo wa darasa na nne umeanzishwa na maafisa wake.

Koskei alisema kuwa mama wa marehemu ambaye hufanya kazi nchini Qatar alikuwa ametumia wazazi wake pesa za kumnunulia mjukuu wao nguo mpya.

Hata hivyo bibi na babu walimtaka mjukuu wao kuwa mvumilivu na kusubiri kupata nguo mpya baada ya Krismasi kwa sababu ya bei ya sasa ya nguo.

“Inakaa alikuwa ameongea na mamaake ambaye alimthibitishia kuwa alikuwa ametuma pesa. Ninadhani alichukulia ombi la subira kutoka kwa nyanya na babu yake kama kukataa kumnunulia nguo mpya,” Koskei alisema.
HII VIDEO ULITAZAMA KAMA BADO CLICK HERE NOW

Nyanyake Rose Ritho akisimulia tukio hilo amesema mkuu wake alijichimbia kaburi kabla ya kukatisha uhai wake.


Alipomuuliza mtoto huyo alimwambia kuwa alikuwa anapanga kupanda mgomba wa ndizi katika shimo hilo.

Nyanya alimuonya na kumtaka alizibe akimwelekezea kuwa ni hatari kuwa na mgomba wa ndizi karibu na waya wa umeme.

Chanzo: Tuko News
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top