MWANAFUNZI UDOM AJIRUSHA GHOROFANI

0

 Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wa Shule ya Uuguzi na Afya ya umma (SoNPH) Ezekiel Sostenes amelazwa hospitali ya Rufaa ya Kanda ya kati Benjamin Mkapa baada ya kujirusha ghorofani.


Awali kabla ya tukio hilo jana, kulikuwa na ujumbe wa WhatsApp ambao Mwananchi imeuona, uliosambaa mitandaoni ukionyesha majibizano kati ya mwanafunzi huyo akimlalamikia mkufunzi wake kuwa alimfelisha kwa makusudi.

Akizungumza na Mwananchi Desemba 15, 2022 Dk Winnie Msangi kutoka hospitalini hapo amesema walimpokea mwanafunzi huyo jana akiwa kwenye hali mbaya.

Winnie amesema Ezekiel anaendelea na matibabu baada ya kupata majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake.

Alipoulizwa kuhusu tukio hilo ofisa habari wa Chuo cha UDOM, Beatrice Mtenga amesema kuwa hana taarifa za tukio hilo na kuomba kupewa muda wa kulifuatilia.

JE! ULITAZAMA VIDEO HII! KAMA HUJATAZAMA BOFYA SASA
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top