MWEKEZAJI ATUHUMIWA KUBAKA KUTEKA NA KUCHOMA NYUMBA ZA WANANACHI MORO

0

Katika hali isiyokuwa ya kawaida wakazi zaidi ya 700 wanaoishi eneo la Kiengea Manispaa ya Morogoro wameangua vilio mbele ya mkuu wa mkoa Bi Fatma Mwasa wakilalamika kuwepo kwa kundi la watu wanaowateka kisha kuwafanyia vitendo vya kikatili ikiwa ni pamoja na kuwabaka.

Picha kutoka Maktaba

Wakizungumza mbele ya RC Mwasa wakazi hao wemesema watu hao wakiongozwa na mtu anayejulikana kwa jina la Jero ambaye ni mwekezaji na msimamizi wa shamba la Tungi Estate wamekuwa wakifika katika makazi ya wananchi hao nyakati za usiku wakiwa na gari la rangi ya bluu na kuwateka, kuwapiga na kuwabaka huku wengine wakilalamika kuingiliwa kinyume na maumbile.

Wakazi hao wamedai kuwa tukio la mwisho lilitokea Disemba 21 ambapo kikundi hicho kikiongozwa na Jero kilifika katika familia ya Bwana Edward na kuwafunga kamba mikononi na vitambaa midomoni kisha kuanza kuwapiga na baadaye walimwagia petroli na kuichoma nyumba yao moto huku mama wa familia hiyo akibakwa na kuingiliwa kinyume cha maumbile.

Miongoni wa wahanga wa tukio hilo ni Aisha anasema siku ya tukio watu hao walifika usiku na mara baada ya kuwateka na kuchoma nyumba moto walimuweka pembeni na kuanza kumbaka kwa zamu na baada ya kumaliza walimuwekea mchanga na majani sehemu za siri.

Imeelezwa kuwa wuwekezaji huyo amekuwa akifanya vitendo hivyo akiwashutumu wakazi hao kufanya shughuli za kilimo na makazi katika eneo analodai ni eneo lake.

Kufuatia hilo mkuu wa mkoa wa Morogoro Fatma Mwasa akatoa siku saba kwa jeshi la polisi mkoa wa Morogoro kumtafuta Jero na kundi lake huku alisisitiza Jero kuondoka katika mkoa huu wa Morogoro huku akiahidi kufuatilia mwenendo wa kesi za wakazi hao.

Aidha RC Mwasa alimtaka Kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro Fortunatus Musilim kueleza hatua alizochukiwa kufuatia tukio hilo ambapo alisema kuwa alipokea taarifa ya tukio hilo baada ya kupigiwa simu na mwandishi wa habari akiwa Dodoma ambapo ameahidi kufuatilia tukio hilo.
Chanzo;Wasafi fm

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top