MZEE ATAKA ARUDISHIWE MAHARI BAADA YA KUGUNDUA MTOTO SIO WAKE

0

 


Mzee mwenye umri wa miaka 78 ameumia moyoni baada ya kugundua kuwa mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 49 si wake kibayolojia na sasa anadai mahari aliyomlipia mkewe.


Wilson Shirichena kutoka Mhondoro nchini Zimbabwe ambaye aliamini kuwa Milton Shirichena alikuwa mwanawe wa kumzaa kwa miongo minne iliyopita, bado yuko katika mshtuko kufuatia ugunduzi huo wa kushangaza.


Vyombo vya habari nchini humo viliripoti kwamba Wilson alidai kwamba Milton alidhaniwa kuwa “mwanawe” alitembelewa na babake halisi, ambaye alimwambia kwamba alikuwa mwanawe kabla hajafa.


Sasa anadai mahari kutoka kwa Milton kwani wakwe zake wote tayari wameaga dunia.


Kwa maneno yake alisema; “Nilipoambiwa hivyo, niliumia sana moyoni kujua kwamba mke wangu mpendwa angenificha kwa miaka 43. Sasa nadai nilipwe pesa zangu za mahari kutoka kwa Milton kwa vile nililipa uharibifu ambao ulipaswa kulipwa na baba yake mzazi, ambaye alimpa mimba mke wangu kabla hatujaoana. “Mke wangu hajisikii vizuri. Ana matatioz ya akili, na wakwe zangu wote walikufa. Kwa hiyo Milton anapaswa kunilipa pesa zangu badala ya baba yake.”


 Alisema; “Siwezi kukataa kwamba kuna maneno yanaenea kuwa mimi si mtoto wa Wilson, lakini hatujawahi kuzungumzia jambo hilo, ikiwa ana uthibitisho wa anachokisema basi afuate taratibu zinazopaswa kufanywa kuliko kukimbizana na mimi kutoka kwa familia kama mbwa."


TUKO.co.ke iliripoti kuhusu kisa sawia na hicho ambapo mwanamume wa miaka 52 wa Bungoma alielekea kortini akitaka waliokuwa wakwe zake kushurutishwa kurejesha mahari yake baada ya ndoa yake na binti yao kugonga mwamba.


Wilberforce Saenyi Murunga alimuoa Irine Mitekho Khaoya miaka minne iliyopita na alitarajia ndoa yao itakuwa ya raha. Mwanamume huyo alisema mama mkwe wake Florence Khaosa, mwanawe Edwin Khaoya pamoja na jamaa zao waifika kwake kuchukua mahari na kutia saini zao kwenye makubaliano ya malipo. Hata hivyo, mwaka mmoja na nusu baadaye, ndoa yao ilianza kusambaratika baada ya mke kudaiwa kuanza kuwa na mipango ya kando. Hii ilikuwa baada ya Murunga kusafiri hadi Marekani kwa masomo zaidi lakini akasema alilazimika kukatiza shughuli hiyo baada ya mkewe kumwarifu arejee nyumbani ili wapate watoto.


“Mke wangu ndiyo sababu ya mimi kurudi kutoka Marekani baada ya miaka miwili, nilikuwa namtumia pesa, lakini aliponiambia nirudi nyumbani tuzae sikuwa na jinsi zaidi ya kurudi nyumbani,” alisema Murunga.

Chanzo:Tukonews

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top