NGOMBE 306 ZILIZOINGIA HIFADHINI KUTAIFISHWA MULEBA

0

Katibu tawala wa Mkoa wa Kagera Toba Nguvila amemtaka kaimu Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Kemilembe Lwota pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama, kuchukua hatua kali ikiwamo kutaifishwa kwa ng'ombe 309 waliokamatwa katika hifadhi ya Luiga iliyoko katika wilaya hiyo, kinyume cha sheria.


Akizungumza baada ya kukamatwa kwa ng'ombe hao katibu tawala huyo amesema kuwa, serikali haiwezi kuwakalia kimya wananchi wanaovunja sheria kwa makusudi kwa kuingiza mifugo katika hifadhi, maana vitendo hivyo vinasababisha uharibifu mkubwa wa mazingira

"Mifugo yote hii iliyokamatwa wahusika wachukuliwe hatua kali za kisheria, kama ni kutaifishwa ng'ombe hawa wote wataifishwe, na kama ni kuwapiga mnada wanadishwe, kwa sababu huu ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu" amesema Nguvila

"Zoezi hili ni endelevu na kama mnavyoona hawa ng'ombe tumekwishawakamata, na tunakwenda kuwataifisha wala hakuna kinyume na hapo, kwa hiyo wanaoendelea na vitendo hivi wajipange wakijua kwamba serikali ipo kazini na iko makini" amesema Kemilembe Lwota kaimu mkuu wa wilaya Muleba

Kwa upande wake mhifadhi wa misitu kutoka wakala wa huduma za misitu nchini - TFS - Wilaya ya Muleba, Mashaka Mrisho amesema kuwa walipata taarifa kuwa katika hifadhi hiyo kuna mifugo na kuamka saa tisa usiku na kuanza kuwasaka, na kwamba ilipofika saa 11 alfajiri walifanikiwa kuwapata

"Hii mifugo wenyewe walikimbia hatujafanikiwa kuwakamata, kwa hiyo tulichofanya ni kuisogeza hapa kituo cha polisi Kasindaga, kwa ajili ya taratibu nyingine za kisheria" amesema Mrisho.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top