RAIS AOMBA APEWE NAFASI NYINGINE AWATUMIKIE WALIMU

0

 

Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) aliyesimamishwa Leah Ulaya amerudishwa kwenye nafasi yake  Ijumaa Desemba 16, 2022.


Ulaya amerejeshwa kwenye nafasi hiyo baada ya kupewa nafasi kujitetea kwa wajumbe wa mkuano mkuu wa CWT unaofanyika jijini Dodoma.

Wakati wa utetezi wake wa kwa nini arudishwe kwenye nafasi hiyo, Ulaya amesema kuwa uamuzi wa kumwondoa ulikuwa wa uonevu.

Awali wakati akiingia ukumbini, baadhi ya wajumbe walikuwa wanaimba wimbo wa ‘Mlete Mzungu’ na wimbo wa mshikamano.

Ulaya ametumia dakika 14 kutoa utetezi mbele ya wajumbe huku akiomba kurejeshwa ambapo baada ya kumaliza, wajumbe hawakuwa na swali la kumuuliza ndipo akaelezwa kutoka nje na wajumbe wakahojiwa wengi wakasema arudishwe, huku sauti chache zikisema asirudishwe na Mwenyekiti akasema waliosema arudishwe wameshinda.

Muda mfupi, Ulaya aliitwa tena ukumbini akisindikizwa na kundi la wajumbe waliokuwa wakiimba nyimbo za kumsifu wakitaka akalie kiti.

Akitoa neno la shukrani mbele ya wajumbe Ulaya amesema, "Nimekaa nje kwa mwaka mmoja na nusu, nipeni nafasi niwatumikie, naahidi kuvunja makundi na kutanguliza maslahi ya walimu mbele, sina kinyongo na mtu yeyote zaidi ya kuchapa kazi.
BOFYA VIDEO HII KUTAZAMA KINACHOENDELEA
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top