Nchini Tanzania kwa sasa ukitamka neno UTAPELI mtandaoni utasikia Kalynda;Kwa kipindi kirefu nimekuwa nikisikia utapeli mtandaoni lakini niliamua kuanza kujikita huko kujua hali ikoje! na utapeli unafanyikaje mtandaoni.
Katika Makala hii fupi nitakueleza zaidi kuhusu Unaodaiwa UTAPELI MTANDAONI unaotokana na namna ya uwekezaji mtandaoni wengine wanaita upatu mtandaoni au ULAGAI mtandaoni.
Baada ya uchunguzi wa muda mrefu na kunilazimu kufanya uchunguzi kwa vitendo nimebaini mambo kadhaa ambayo kamwe hiki kinachoitwa ULAGAI hakiwezi kuisha na kitaendelea licha ya baadhi ya watu kuishia kupata hasara mtandaoni lakini wengine wakinufaika na mfumo huo unaoitwa Ulagai.
Baada ya kujiunga na APP mbalimbali na Tovuti mbalimbali zinazoeleza kuwa unajipatia faida kwa kuwekeza katika mtandao husika nimebaini kuwa
MOSI;Faida inayozalishwa na kupewa mtu ni ile inayotokana na watu kuendelea kujiunga nyuma yaako na kadri watu wanavyoendelea kujiunga ndivyo Kampuni/Jukwaa hilo linavyoendelea kustawi na kukaa kwa muda mrefu tofauti na Majukwaa ambayo yanakosa washiriki wanaowekeza pesa zao.
PILI;Tanzania licha ya Majukwaa mbalimbali amabyo yalijitangaza na mwishoni kupotea bila kujua hatima za wawekezaji wake kujua hatima yao huko katika mataifa ya wenzetu hivyo vitu viko huru sana sawa na kucheza game mtandaoni au Kasino mbalimbali au maguruguru hivyo biashara hizo husambazwa katika mataifa mbalimbali ikiwemo nchini za Africa ambazo bado hajakua kiteknolojia.
TATU;Kwanini watu wanaendelea kuwekeza licha ya kushindwa kupata faida mtandaoni? Uchunguzi wangu umebaini kuwa Kuna watu wao ni kutafuta TEAM ambayo yeye huwa mtu wa Kwanza kupata link/kiungo na kusambaza kwa team yake wakijiunga ndivyo anavyozalisha zaidi na hapo walioko nyuma yake hupambana nao waweze kupata wawekezaji,hali ambayo mwishoni ambao hukosa faida ni wachache kuliko wengi waliopata faida.
NNE;Ajira katika mazungumzo na watumiaji wa Majukwaa hayo maneno yao ni kwamba wewe endelea kudai utapeli wakaati wenzako wanawekeza,na hapa nimekutana na watu wenye mitaji au biasharaa kubwa wakijiunga na kukuza mitaji yao kwa muda mfupi na kutoa hivyo kuchangia watu kuendelea kutumia fursa mtandaoni.
Kwa leo naomba nieleze haya mengine yataendelea kuelezwa siku hadi siku kadri ninavyoendelea kuzitumia fursa hizi na kuendelea kuchunguza ikiwa je zimewasaidia wanaojiunga au zinawarudisha nyuma!.
KWA KUMALIZA TAZAMA VIDEO HII KUCHUNGUZA JUKWAA UNALOTUMIA KABLA YA KUWEKA HELA YAKO MTANDAONI.