Shirikisho la Jumuiya za Watu Wenye Ulemavu Zanzibar (Shijuwaza) limetoa misaada wa vyakula kwa watu sita (6) wenye ulemavu Kisiwani Pemba, kwa lengo la kuwasaidia watu wenye ulemavu kutokana hali duni walizonazo ikiwa ni shamra shamra za kuelekea maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu duniani.
Akikabidhi misaada hiyo Mwenyekiti wa Shijuwaza Bi. Mwamdawa Khamis Mohammed, amesema watu wenye ulemavu wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo hali duni za kimaisha, makaazi duni sambamba na kukosa shughuli za kufanya, hivyo basi kuna kila sababu ya kuwasaidia watu wenye ulemavu ili kuweza kuwafariji.
"Kama tunavyua ndugu zangu kuwa December 03, tunakwenda kwenye maadhimisho ya siku ya wenye ulemavu duniani, hivyo basi katika kuelekea maadhimisho hayo tunapaswa kuwatembelea ndugu zetu wenye ulemavu mbali mbali kuwapa taarifa hizi pamoja na kuwafariji ili nao wajione ni sehemu ya Jamii" Mwenyekiti Shijuwaza
Sambamba na kutoa misaada hiyo, amewaomba watu wenye ulemavu Kisiwani Pemba kujiunga na na mshirikisho pamoja na jumuiya mbali mbali za watu wenye ulemavu ili waweze kutambuliwa na kupatiwa haki zao za msingi ikiwemo mafunzo mbali mbali ya ujasiriamali pamoja mikopo ili waweze kufanya biashara ndogo ndogo zitakazoweza kuwasiadia katika kukabiliana na hali ngumu walizonazo.
"Ni waombe sana ndugu zangu kujiunga na mashirikisho pamoja na jumuiya mbali mbali za watu wenye ulemavu ili muweze kutambuliwa na mupatiwe stahiki zenu, kama vile vitambusho, mafunzo mbali mbali ya ujasiriamali pamoja na mitaji ya biashara Ili muweze kujikwamua katika hali duni mulizonazo" aliwaonba
Mwenyekiti wa Shijuwaza Bi. Mwamdawa, akikabidhi msaada wa chakula kwa Bi. Time Ramadhan Juma 45, ambaye ni mlemavu wa viungo anayeishi Shehia ya Majenzi Micheweni.
Kwa upande wake, mjumbe wa kamati tendaji Taifa wa Shijuwaza Feisal Abdalla Said, amesema miongoni kwa sababu zinapelekea watu wenye ulemavu kuwa na Hali duni ni kukosa shughuli za sahihi za kufanya, jambo ambalo linawafanya kuwa tegemezi kwa familia zao.
"Unajua tatizo sio kuwa na ulemavu kwasababu Kila mmoja ni mlemavu mtarajiwa na ulemavu anatoa Mungu na rizki anatoa Mungu, lakini kikubwa kinachowakabili ndugu zetu hawa ni kukosa shughuli sahihi za kufanya ikiwemo kujishusha na biashara ndogo ndogo" alisema
Wakitoa neno la shukurani baada ya kukabidhiwa misaada hiyo, wamewaomba viongozi hao kuwa Karibu nao Ili waweze kufahamu changamoto mbali mbali wanazopitia Ili kuzipatia ufumbuzi.
Bi. Time Ramadhan Said, Mwenye ulemavu wa viungo, akitoa neno la shukurani kwa viongozi wa Shijuwaza baada ya kupokea msaada wa chakula.
Msaada huo wa vyakula imetolewa na Shirikisho la Jumuiya za Watu Wenye Ulemavu Zanzibar (SHIJUWAZA) kwa kushirikiana na baraza la taifa la watu wenye ulemavu Zanzibar, ambapo watu sita (6) wenye ulemavu kutoka Wilaya ya Chake Chake na Micheweni walipatiwa msaada wa Mchele, Unga pamoja na Sukari.
Mwenyekiti wa Shijuwaza Bi. Mwamdawa, akikabidhi msaada wa chakula kwa Bi. Sakina Khamis Mbarouk, ambaye ni mama mzazi wa watoto wenye ulemavu wa viungo ambao ni Kassim Omar Juma mwenye umri wa miaka 22 na Aisha Omar Juma mwenye umri wa miaka 3 na miezi 5, katika Kijiji cha Ingadungu Shehia ya Mfikiwa.
Ndugu wa Riziki Omar Kombo 22, mwenye ulemavu wa viungo katika Shehia ya Majenzi Wilaya ya Micheweni, akipokea msaada wa vyakula kutoka kwa uongozi wa Shijuwaza.