WAKUFUNZI KUTOKA 'OMPR' WAWAPIGA MSASA WAJUMBE WA KAMATI ZA MAENDELEO YA JIMBO PEMBA, KUANDAA RIPOTI.

Hassan Msellem
0

Wajumbe wa kamati za maendeleo ya majimbo Kisiwani Pemba wameombwa kuibua miradi ya maendeleo ambayo inakwenda sambamba na kiwango cha fedha kilichotengwa katika kuzisaidia kamati hizo.



Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Uratibu wa shughuli za Serikali kutoka Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar, Bi. Siajabu Suleiman Pandu huko katika Ukumbi wa Jamhuri Holl Wete katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wasimamizi wa kamati za Maendeleo za Jimbo Mkoa wa Kaskazini Pemba, amesema kuwa uibuaji wa miradi ambayo bajeti yake inazidi kiwango cha fedha kilichotengwa katika kuzisaidia kamati hizo inapelekea kutokukamilika kwa wakati miradi hiyo jambo ambalo linapelekea ripoti mbaya Kwa kamati hizo.


Aidha Mheshimiwa Siajabu, amewaomba wajumbe wa kamati hizo kuwa wazalendo katika utekelezaji wa miradi hiyo ili kuhakikisha lengo la kuanzishwa kamati hizo linafikiwa.


Nae, Afisa Uratibu wa Shughuli za Serikali Kisiwani Seif Faki Juma, amewataka wajumbe wa kamati hizo kuwasilisha muhtasari wa vikao vya uibuaji wa mradi kutoka kwa wananchi ili kuepukana na mapungufu yanayoweza kujitokeza.

Kwa upande wake, Afisa miradi kutoka Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Bi. Mariam Omar Hamad, kutokuwasilishwa kwa taarifa za fedha za mfuko wa maendeleo ya Jimbo ni miongoni mwa mapungufu yaliyojitokeza katika ripoti za mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali katika miradi inayotekelezwa na kamati hizo, hivyo basi amewaomba wajumbe wa kamati hizo kuwasilisha taarifa zao za fedha za mfuko wa maendeleo ili kuepukana na mapungufu hayo.

Nao wajumbe wa kamati hizo wameombwa kuongezewa kiwango cha fedha katika utekelezaji wa miradi ili kuondokana na changamoto ya rasilimali fedha inayowakabili. 

Mafunzo hayo ya siku mbili yametolewa na wakufunzi kutoka Ofisi ya makamo wa Pili wa Rais Zanzibar, kwa wajumbe wa kamati za maendeleo ya Jimbo Kisiwani Pemba katika kuwajengea uwezo wajumbe wa kamati hizo kuandaa marejesho ya ripoti katika shughuli mbali mbali wanazozifanya.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top