Walinzi watatu wa kampuni tofauti wamekutwa wameuawa katika sehemu zao za kazi usiku wa kuamkia Desemba 22,2022 katika mtaa wa Shilabela kata ya Buhalahala mjini Geita
Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Shilabela Bw Fedrick Masalu amefika kwenye eneo la tukio na kuwataja walinzi hao waliouwawa kuwa ni Charles Shija ,Jumanne Shabani na Henry Selestine huku akiwaomba wananchi kuwa na utulivu katika kipindi hiki kigumu ambapo Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi zaidi wa tukio hilo.
Chanzo;
stormfmtz