Jeshi la Polisi Mkoani Kagera linawashikilia watu watano kwa kosa la kuiba mtoto mchanga tukio lililotokea Desemba 01, Mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa polisi Mkoani humo Kamishina msaidizi wa polisi William Mwampaghale mjini Bukoba, ameeleza kuwa mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Benita Beneti mwenye umri wa Mwezi mmoja aliibwa nyumbani kwao na Watu waliokwenda kumtembelea Johanitha Augustino ambaye ni mama wa mtoto huyo nyumbani kwake Migera Manispaa ya Bukoba.
Kamanda Mwampaghale amefafanua kuwa badaa ya kuripotiwa kwa tukio hilo, jeshi la Polisi lilianza msako mkali ambapo kuanzia tarehe 02 hadi 08 Desemba mwkaa huu watuhumiwa hao walianza kukamatwa kwa nyakati tofauti katika maeneo ya mkoa wa Kagera na Jijini Dodoma.
"Mtoto huyo baada ya kuibwa na watuhumiwa hao walimchukua na kwenda nae kwa mganga wa Kyenyeji kamachumu wilaaynai Muleba ILI afanyiwe dawa asimsumbue aliyemchukua." Amesema Mwampaghale.
SASA UNAWEZA KUTUMIA TOVUTI HII KUJIPATIA PESA MTANDAONI.
Ameongeza kuwa msako wa watuhumiwa hao uliendelea na tarehe 08/12/2022 muda wa saa 12:00 jioni mtuhumiwa aliyekuwa ameondoka na mtoto alikamatwa Jijini Dodoma akiwa na mtoto huyo, na kuongeza kuwa Afya ya mtoto huyo inaendelea vizuri na tayari amekabidhiwa kwa mama yake huku akiwa chini ya uangalizi.
Aidha ameongeza kuwa watuhumiwa wote wamehojiwa na kukiri kutenda kosa hilo na watafikishwa mahakamani mara baada ya taratibu za kiupelelezi kukamilika.
Sambamba na hayo jeshi hilo limetoa wito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano katika jitihada za kupambana na ukatili kwa watoto huku likitoa onyo kwa kwa watu wote wanaoendekeza vitendo vya ukatili kuacha mara Moja.