Watu wawili wa Kijiji cha Kimana Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, Jackson Farao Njoliba (25) na mwenzake Harwon Japhet (32) wamehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kosa la kumlawiti Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 10 kwa kupokezana.
Mahakama imesema tukio hilo lilitokea April 23,2022 katika Kijiji cha Kimana Kiteto ambapo baada ya kumlawiti Mtoto Watuhumiwa hao wakamfungia ndani Mtoto huyo kwa siku nzima hadi alipokuja kufunguliwa na Mtoto mwenzake aliyefika nyumbani kwa Mtuhumiwa Jackson Farao Njoliba (Rasi) baada ya kusikia kelele ndani.
CC;Millardayo
ULITAZAMA VIDEO HII KAMA BADO BOFYA SASA