WANACHAMA WAWILI WA 'ACT' WAZALENDO WASHIKWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA KUSINI PEMBA, KWA TUHUMA ZA KUTOA KAULI ZA KUKASHIFU NA UCHOCHEZI.

Hassan Msellem
0


Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, linawashikilia wanachama wa Wiwi wa Chama Cha  ACT  Wazalendo ambao ni Salim Abdalla Herezi Mwenye umri wa miaka 65, mkaazi wa Mjimbni Mkoani, ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya uongozi Jimbo la Mtambile na Nachia Ali Jamal 39, mkaazi wa Wambaa Mkoani, ambaye ni mjumbe wa kamati ya fedha Jimbo la Chambani kwa tuhuma za kutoa maneno ya kuwakashifu viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, pamoja na kutoa maneno ya uchochezi.


Akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari katika ofisi za makao makuu ya Jeshi Hilo Madungu Chake Chake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Kamishna msaidizi wa Polisi Abdalla Hussein Mussa,  huko Ofsini za Polisi Madungu Chake Chake, amesema wanachama hao walidaiwa kufanya makosa hayo wakiwa katika kikao cha ndani cha chama cha ACT Wazalendo, wakati wakitoa maoni kuhusu uteuzi wa Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi Zanzibar Ndugu. Thabit Idarous Faina aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa mkurugenzi wa tume hiyo.


"Ndugu wanahabari mnano tarehe 10 mwezi December mwaka huu kwa nyakati tofauti usiku Jeshi la Polisi mkoa wa Kusini Pemba, limewakamata na kuwahoji watu wawili kuhusiana na n kutoa maneno ya uchochozi matusI kwa viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kupinga uteuzi wa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar 'ZEC' ndugu Thabit Idarous Faina, watu hao ni wanachama wa chama cha ACT Wazalendo, wa kwanza ni ndugu Salum Abdalla Herezi, maarufu wa jina la mwalimu Herezi mwa 65, ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya uongozi Jimbo la Mtambile mkaazi wa Mjimbini Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba na Nachia Ali Jamali 39, ambaye ni mjumbe wa kamati ya fedha Jimbo la Chambani na mkaazi wa Wambaa, tayari wamehojiwa na kuachwa huru huku upelelezi dhidi ya tuhuma hizo unaendelea na mara Jeshi la Polisi litakapokamilisha upelelezi wa shauri hili mara moja tutawafikisha mahakamani katika hatua nyengine za kisheria" alisema Kamanda huyo.


Aidha Kamanda Abdalla, ameongeza kuwa mnamo December 05, mwaka huu Majira ya saa 4:30 hadi saa 6 za mchana huko Mtambile katika Ukumbi wa Ofisi za chama Cha ACT Wazalendo jimbo la Mtambile wakiwa kwenye kikao cha ndani cha chama ACT Wazalendo uchochozi Kwa viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Kisha kutuma kwenye mitandao ya kijamii.


Sambamba na hayo Kamanda Abdalla,  ametoa wito kwa viongozi wa vyama vya Siasa kutumia vyema uhuru na fursa za kufanya vikao vya ndani vya chama kwakufuata Sheria, kanuni na taratibu kinyume na kutumia Lugha za matusi Kwa viongozi wa Serikali na vyama vyengine.


Hata hivyo, Kamanda huyo amesema Mkoa huo upo salama kutokana na wananchi kuwana mashirkoano na Vyombo vya Ulinzui na Usalama kwenye Mkoa huo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top