WANAFAMILIA WATATU WAFARIKI AJALI YA MOTO

0

 


Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Watoto watatu wa familia moja ya Mathayo Samson katika mtaa wa Igomelo kata ya Malunga Manispaa ya Kahama wamefariki dunia kufuatia ajali ya moto.

Tukio hilo limetokea leo Novemba 30, 2022 majira ya saa kumi na moja alfajiri ambapo moto uliunguza nyumba ya Mathayo Samson na kusababisha vifo vya watu watatu wakiwemo wanafunzi wawili.

Akizungumzia ajali hiyo Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna msaidizi wa Polisi Janeth Magomi ambaye ameeleza juu ya tukio hilo huku akithibitisha vifo vya watu watatu waliofariki katika ajali hiyo ya moto.

“Leo tarehe 30 mwezi wa 11 ilikuwa majira ya saa kumi na moja asubuhi katika mtaa wa Igomelo kata ya Malunga Manispaa ya Kahama Mkoa wa Shinyanga nyumba ya ndugu Mathayo Samson ana umri wa miaka 39 na mfanyabiashara nyumba yake iliwaka moto na madhara yaliyosababisha ni vifo vya watu watatu”,amesema Kamanda Magomi.

Waliofariki dunia katika ajali hiyo ni Dotto Juma mwenye umri wa Miaka 33 mkulima, Samson Mathayo mwenye umri wa Miaka 13 mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi ST. Antony of Padua pamoja na Joseph Samson mwenye umri wa miaka 7 mwanafunzi wa darasa la pili shule ya msingi ST. Antony of Padua.

Kamanda Magomi amesema jeshi hilo kwa kushirikiana na jeshi la zimamoto na uokozi limefanikiwa kufika katika eneo la tukio na kwamba jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top