WANAUME KUWENI NA HOFU YA MUNGU MSIBAKE WATOTO!

0
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nice Munissy akizungumza kwenye kikao hicho.

 

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

SHIRIKA la Women Elderly Advocacy and Development Organization (WEADO) limefanya kikao cha uchechemuzi na Kamati za MTAKUWWA Kata za Masengwa, Tinde na Wilaya, wilayani Shinyanga kujadili na kuweka mikakati namna ya kuzuia mimba na ndoa za utotoni.


Kikao hicho kimefanyika leo Desemba 8,2022 katika ukumbi wa mikutano Shule ya Sekondari ya wasichana Tinde, huku Mgeni Rasmi akiwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nice Munisy.

Afisa miradi kutoka Shirika hilo la WEADO Winnie Hinaya, amesema wamefanya kikao hicho ili kujadiliana na kubadilishana uzoefu na Kamati za Mtakuwwa, katika kuendeleza mapambano ya kuzuia ndoa za utotoni.

Amesema mradi huo wa vunja ukimya zuia ndoa za utotoni ni wa miaka miwili ambao utakoma Aprili mwakani,kwa ufadhili wa Shirika la Foundation for Civil Society ambao unatekelezwa katika Kata za Masengwa na Tinde.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nice Munissy, akizungumza wakati akifungua kikao hicho, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia ili yaishe kabisa na jamii kubaki salama.

Amesema katika kuendeleza mapambano hayo ya kupinga ukatili wa kijinsia ikiwamo kutokomeza mimba na ndoa za utotoni, jamii pia inapaswa kuwa na hofu ya mungu, na kuacha kufanya mapenzi na watoto wadogo ambao hawana hisia zozote.

"Ili kumaliza ukatili ndani ya jamii pia tunapaswa kumshirikisha Mungu, haiwezekani Mwanaume mzima una kwenda kumbaka mtoto wa miaka sita ambaye hana hata hisia zozote sasa anapata raha gani silaana tu,"amesema Munissy.

Katika hatua nyingine Munissy, amewataka pia watoto pale wanapoona viashiria vya kufanyiwa vitendo vya ukatili, wasisite kutoa taarifa mapema ili wasaidiwe kabla ya kupata madhara, huku akimpongeza mwanafunzi ambaye amekuwa akitoa taarifa juu ya wenzao kufanyiwa vitendo vya ukatili na amempatia fedha Sh.30,000 kwa ajili ya kununua vifaa vya shule.


Kwa upande wake Mratibu wa Dawati la Jinsia kutoka Polisi Mkoa wa Shinyanga Monica Venance, amewasihi wazazi washirikiana na vyombo vya dola pale zinaporipotiwa kesi za ukatili, na siyo kumalizana kimya kimya na watuhumiwa na kusababisha kesi kufutwa na hatimaye ukatili kuendelea ndani ya jamii.
Chanzo;Malunde1 Blog
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top