Watu wenye ulemavu wa kuona mkoani Mbeya wamedai kukosekana kwa maandishi ya nukta nundu kwenye mipira ya kiume (kondom) kunawaweka kwenye hatari ya kupata magonjwa ya zinaa na mimba zisizotarajiwa

Wameibua hoja hiyo wakati wa kikao cha kamati ya watu wenye ulemavu cha kujadili changamoto na kuweka maazimio ya kukabiliana nazo kwa mwaka ujao ambacho kiliwahusisha wadau mbalimbali chini ya uratibu wa shirika lisilokuwa la kiserikali la Child Support jijini Mbeya
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu mkoani Mbeya, Luka Mahenge amesema kuwa kuna uwezekano jamii ya watu wasioona kutumia mipira ya kiume ambayo imeisha muda wake jambo ambalo ni hatari kwa afya zao
Nae mkurugenzi mtendaji wa shirika la Child Suport Tanzania, Noela Msuya amesema wakiwa wadau wa mambo ya ustawi wa jamii wanawajibu wa kutoa msukumo kwa mamla za serikali kutekeleza sera na kutatua changamoto za watu wenye ulemavu
Miongoni mwa maazimio yaliyoweka na kamati ya watu wenye ulemavu mkoani Mbeya kwa mwaka ujao ni pamoja na kufuatilia miundombinu rafiki ya watu wenye mahitaji maalum kwenye majengo yan umma na binafsi.
Chanzo;Eatv