AMCHINJA NA KUMTUPA MTONI MKEWE AKIMTUHUMU KUCHEPUKA

0

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia, Mapinduzi Siliya (45) kwa tuhuma za kumuua mkewe, Terezia Mtajiha.


Siliya anadaiwa kumchinja kwa kutumia kisu kisha mwili kuutupa mto Nzovwe jijini humo.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Benjamin Kuzaga amesema tukio hilo limetokea jana Jumatano  Januari 11, 2022   na kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya kwa uchunguzi wa kitabibu.


Kuzaga amesema kisa cha mauaji hayo ni mtuhumiwa kumtuhumu mke wake kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine.

"Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kwa kushirikiana na wananchi na wadau wengine katika kubaini, kuzuia uhalifu ili kila mtu afanye shughuli zake katika hali ya amani," amesema Kuzaga.

Wilisi Kupasya jirani wa familia ya Siliya amesema wawili hao walikuwa na ugomvi wa mara kwa mara hasa walipokuwa wanatoka kwenye starehe zao.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top