ANGEL AUAWA KWA KUNYONGWA NA WASIOJULIKANA MWILI WATUPWA.

0

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Waziri Kindamba ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani Songwe kuhakikisha linawasaka na kuwakamata watu waliohusika katika tukio la mauaji ya mfanyakazi wa TANESCO aitwaye Angel Shakinyau (33) aliyeuawa usiku wa kuamkia Januari 16, 2022 na mwili wake kutupwa jirani na nyumba anayoishi.

PICHA KUTOKA MAKTABA
Marehemu Angel Shakinyau anadaiwa kuvamiwa usiku wakati akirudi nyumbani kwake na kisha kuuawa kwa kunyongwa na kamba inayodaiwa kuchanwa kwenye turubai ya Bajaji.


Mwili wa marehemu umeagwa katika makazi yake mjini vwawa na kusafirishwa kwenda mkoani Dodoma Kisha kwao Shinyanga kwa ajili ya mazishi.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Waziri Kindamba amewahasa watu wote ambao wanafanya vitendo vya ukatili ndani ya Songwe hawatakuwa salama tena, kwani watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria za Nchi.
KAMA HUKUTAZAMA VIDEO HII TAZAMA SASA
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top