BABA AKUTWA AMEFARIKI BAADA YA KUNYIMWA MKOPO NA MKEWE

0

 Polisi jijini Nairobi wanachunguza kifo cha kutatanisha cha mfanyabiashara maarufu na mwanasiasa wa Tharaka Nithi Francis Kiambi Matanka.

Tharaka Nithi politician Francis Kiambi Matanka.

Mwili wa Kiambi ulipatikana katika kitanda chake nyumbani kwake Karen, Nairobi asubuhi ya Jumatatu, Januari 10 mwaka huu.

 Taarifa mpya zinaonyesha kuwa kabla ya kifo chake, mfanyabiashara huyo alikuwa na tofauti za kinyumbani na mkewe Mary Waigwe Muthoni. 

Kulingana na taarifa iliyowasilishwa katika Kituo cha Polisi cha Karen Muthoni aliwaambia maafisa hao ambao mumewe alikuwa ameomba amhakikishie mkopo wa KSh 2 bilioni lakini akamkatalia.

Imeelezwa kuwa Mkopo huo ulilenga kufadhili biashara yake mpya,Baada ya kutofautiana kwa kukataliwa kupata mkopo huo  wawili hao walienda kulala katika vyumba tofauti vya kulala usiku huo, lakini mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 50 alipatikana akiwa amefariki asubuhi iliyofuata. 

“Kila mmoja alilala katika vyumba tofauti na marehemu hakuzinduka tangu wakati huo, bali alisikika akikoroma na alikuwa akitapika chumbani kwake. Ilikuwa hadi leo (Jumatatu) mwendo wa saa  kumi na mbili alipokwenda kumchungulia marehemu na kumkuta akiwa amekufa juu ya kitanda chake na matapishi kando ya kitanda,” ilisema sehemu ya taarifa ya polisi.

Mwili wa marehemu ulihamishwa hadi Lee Funeral Home ukisubiri kufanyiwa uchunguzi zaidi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top