Braza la Mji Chake Chake limetakiwa kushirikiana na kitengo cha afya na Mazingira ili kuhakikisha hali ya usafi wa mazingira inaimarika zaidi katika kukabiliana maradhi ya mripuko yanayotengeneza kujitokeza.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa mtendaji wa kamisheni ya kukabiliana na maafa Zanzibar Nd. Makame Khatib Makame, huko katika Ukumbi wa baraza la Mji Chake Chake katika ziara ya kutathmini kutokomeza kipindu pindu Zanzibar Kisiwani Pemba, amesema katika ziara hiyo kumebainika changamoto kadhaa ikiwemo kuvuja kwa baadhi ya mabomba ya maji taka, mitaro isiyo na salama pamoja ukosefu wa gari la kubebea maji taka katika baraza hilo.
Kwa upande wake Afisa Afya na mkaguzi wa Afya baraza la Mji Chake Chake Bw. Hassan Haji Hassan, amesema baraza la Mji Chake Chake linakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo, wa vitendea kazi sambamba na ukosefu wa gari la kubebea maji taka jambo ambalo linapekelea changamoto katika kukabiliana usafi wa mazingira katika baraza Hilo.
Aidha, amesema licha ya baraza hilo kukabidhiwa changamoto mbali mbali lakini limefanikiwa kuondosha tani 526 sawa na asilimia 92.8 kutoka tani 5670 walizopanga kuzifikia kutoka mwezi January hadi December mwaka 2022.
Ziara hiyo ililenga kutembelea maeneo mbali mbali yenye miradi ya usafi wa mazingira pamoja na kupokea taarifa ya baraza la Mji Chake Chake kuanzia mwezi January hadi December mwaka 2022.