Mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashimu Mgandilwa @hashimmgandilwa amefanya msako wa nyumba kwa nyumba kwa Wazazi wa Kata ya Chongoleani ambao wameshindwa kuwapekeka Wanafunzi waliohitimu darasa la saba kuripoti Shule kwa lengo la kuanza kidato cha kwanza ambapo Wazazi hao wamekamatwa na watachukuliwa hatua za kisheria.
Mgandilwa amefikia uamuzi huo baada ya kuona idadi ndogo ya Wanafunzi walioripoti Shuleni siku ya Jumatatu katika Shule ya Sekondari Chongoleani ambapo walioripoti ni Wanafunzi 57 tu kati ya Wanafunzi 92 waliotakiwa kuripoti Jumatatu ya tarehe 9 Januari.
Mgandilwa amesema Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ndaoya waliotakiwa kuripoti Shule ni 100 lakini mpaka sasa wameripoti 31 tu huku kwa upande wa Wanafunzi wa darasa la awali idadi ya walioandikishwa kwenye Shule nne za Kata ya Chongoleani ni Wanafunzi 130 lakini mpaka sasa ni Wanafumzi 28 tu walioripoti Shule.
Kutokana na idadi hiyo ndogo ya Wanafunzi kuripoti Shule, DC amelazimika kwenda kuhamasisha nyumba kwa nyumba Katika Kata ya Chongoleani huku akiwakamata Wazazi wasiowapeka Watoto wao Shuleni.
USISAHAU KUTAZAMA VIDEO HII
"Ninalazimika kutembea Mtaa kwa Mtaa na nyumba kwa nyumba kukamata Wazazi walioshindwa kuwapekeka Watoto Shuleni kwani elimu ni bure na Serikali imetoa fedha nyingi kwenye ujenzi wa madarasa ili Wanafunzi waweze kusoma sasa haya madarasa nani anatakiwa kusoma kama sio Mtoto, sitamvumilia Mzazi yeyote kwa hili,"
Chanzo; MILLARDAYO