Mtandao wa IDAWA MEDIA unatoa pongezi kwa mwandishi wa WASAFI MEDIA kwa kutunukiwa tuzo ya uandishi wa habari za watoto mkoani Mbeya,Pia mtandao huu unawapongeza waandishi wengine kutoka vituo cingine mkoani humo waliopata Tuzo.Mwandishi Enock Saimon akipokea tuzo yake!
Waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari Mhe. Nape Nauye, ameongoza zoezi la utoaji wa tuzo za umahiri Kwa wandishi wa habari Mkoani Mbeya za Tulia Trust Journalism Awards, zinazofadhiliwa na Mkurugenzi wa taasisi ya Tulia Trust Dkt. Tulia Ackson.
Tuzo hizo zilizotolewa Kwa mara ya kwanza usiku wa January 7 zimehusha kupima umahiri wa wandishi wa habari katika makundi kumi na nne ya habari mbalimbali ikiwemo habari za Watoto, ambazo Mwandishi kutoka Wasafi Media Mkoa wa Mbeya @enocksaimon amekua mshindi wa kwanza.
Makundi mengine ya habari ni Habari za Jamii, Habari za Afya, Habari za utalii, Habari za mazingira, Habari za Ukatili wa kijinsia, Habari za Madini na gesi, Habari za Kilimo,
Habari za Elimu, Habari za makundi maalum, Habari za uchumi na biashara, Habari za uchunguzi, Habari za siasa na tuzo ya mpigapicha bora.
KAMA HUJA SUBSCRIBE CHANNEL HII UTAKOSA MENGI 2023.