KAKA AHUKUMIWA KULIPA TSH 500,000/ KWA KUMNAJISI DADA YAKE

0

 FRANK Kigomba (31) mkazi wa Kijiji cha Kising'a wilayani Kilolo, amehukumiwa kwenda jela miaka 30 na kulipa fidia ya Sh 500,000 kwa kosa la kumbaka dada yake wa tumbo moja mwenye umri wa miaka 15.


Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi amesema tukio hilo la ubakaji lilitokea Januari 2, mwaka huu na kwamba tayari lilifikishwa mahakamani na hukumu imetolewa.

Bukumbi alisema mtuhumiwa huyo alienda chumbani kwa ndugu yake na kumuita, akimtaka amsaidie kuingiza mbao ndani ya pagale la nyumba anayojenga na kisha akamkamata kwa nguvu na kumvua nguo, kabla ya kumuingilia kwa nguvu na kumsababishia maumivu makali.

"Uchunguzi ulibaini kuwa mtuhumiwa huyo alishauriwa na mganga wa kienyeji kuwa akifanya mapenzi na ndugu yake atapata utajiri, alifikishwa mahakamani na kusomewa shitaka lake na kukiri kosa; na kuhukumiwa kifungo hicho," alisema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top