MAMA AOTA NYAMA KWENYE KIUNO,AOMBA WADAU KUMSAIDIA MATIBABU

0

 Mama mmoja (35) mkazi wa Kitongoji cha Bwahari Pwani, Kijiji cha Imekuwa kata ya Naumbu Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara anaomba kusaidiwa Pesa ili afanyiwe upasuaji wa Nyama iliyomuota kwenye Kiuno na kushuka chini ambapo imefunika Kalio lake la kulia hali inayopelekea kutembea na hata kukaa kwa shida.Akiongea na Faida Online TV baada ya kumtembelea kwenye Kitongoji hicho kilichopo pembezoni mwa Bahari ya hindi, Mama huyo amesema Kinyama hicho kinauma na anakosa raha kwa kuwa anashindwa kufanya kazi zake kama Kilimo na pia anakataliwa na Wanaume huku wakimdhihaki kwa kumuita "Kalio moja”

Hata hivyo amesema Nyama hiyo imemuota tangu akiwa mdogo na inakuwa siku hadi siku lakini hana uwezo wa kufanya upasuaji huku akitegemea huruma ya Walimwengu kumsaidia Pesa ili aondokane na maumivu na fedheha anayoipitia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Ndugu Ismaili Hassani amekili kuwa Mama huyo anateseka hivyo kuomba wenye uwezo waweze kumsaidia kwa kuwa hata Familia yake haijiwezi.

Kwa mawasiliano ya mtu wa Karibu
0688 481 412 AU 0673 152 454
TAARIFA HII NI KWA MUJIBU WA NURUFM,KAMA UMEGUSWA TUNAOMBA CHANGIA KWA CHOCHOTE ,NA MWENYEZI MUNGU AKUSAIDIE.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top