MAMA MBARONI KWA KUMUUA MWANAE WA DARASA LA TATU

0

 Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Mwanamke Joyce Matingo (26) kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wake, Emily Matingo (9) mwanafunzi wa darasa tatu katika shule ya msingi Mnyamwanga Wilaya ya Rungwe mkoani hapa.


Kamanda wa Polis Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga ameliambia Mwananchi  Januari 10, 2023 kuwa tukio hilo limetokea Jumapili Januari 8 mwaka huu majira ya saa 12.00 jioni baada ya mtuhumiwa kudai kuwa mwanaye aliiba Sh40, 000.

Imedaiwa kuwa mtuhumiwa alimfunga kamba miguu na mikono manaye na kisha kumshambulia kwa kipigo sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababisha kifo.

Kwa mujibu wa Polisi, mtuhumiwa alidai kuwa mwanaye awali aliiba Sh 16,000 na ndipo alipofikwa na hasiri na kuchukua uamuzi huo.

“Kitendo kilichofanywa cha kinyama kwani kabla ya kutekeleza kitendo hicho alimfunga kamba miguu na mikono na kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake kitendo ambacho ni cha kinyama na hakivumilikia,” amesema.

USIPITWE NA VIDEO HII MUHIMU UTAZAME


Kuzaga amesema mtuhumiwa alipohojiwa na polisi amekiri kuhusika na tukio hilo na kwamba kwa atafikishwa Mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.

“Natoa wito kwa wazazi kauchana na tabia ya kufanya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanapo watuhumu kufanya matukio ni vyema kutoa taarifa katika vyombo husika,” amesema.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top