MBARONI KWA KUIBA POMBE

0

Mahakama ya Nakuru imeruhusu polisi kuwazuilia zaidi wanaume wawili wanaotuhimiwa kuiba bidhaa zenye thamani ya shilingi milioni 15 kutoka kwa kampuni ya kuagiza na kuuza pombe.


Mnamo jioni ya Ijumaa - Januari 20 - Hakimu Mkuu wa Nakuru Bildad Ochieng aliruhusu polisi kuwazuilia kwa siku tatu zaidi Polycarp Oketch na Emmanuel Onyango katika kituo cha polisi cha Nakuru. 

Oketch alikuwa ameandikwa kama afisa wa mauzo huku mwenzake - Onyango - akiwa dereva. 

Wanadaiwa kuiba bidhaa hizo wakati wa msimu wa Krismasi,Walikamatwa mnamo Januari 14, 2023 kutoka eneo walilokuwa wamejificha na wamekuwa wakizuiliwa tangu siku hiyo. 

"Wawili hao watafikishwa mahakamani mnamo Jumatatu januari 23,2023 ili kusomewa mashtaka. 

Hakimu Oching aliambiwa kuwa polisi walihitaji kupata taarifa kutoka kwa Benki ya Prime ili kuwasaidia katika uchunguzi wao. 

Afisa wa uchunguzi Wilfred Kinyua alimwambia hakimu kuwa wanahitaji taarifa ya benki ili kuthibitisha jinsi wawili hao walivyofanya biashara kabla ya kutoweka na bidhaa hizo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top