MBARONI KWA KUVUNJA SAHANI ZA MAMA MKWE WAKE

0

 Mahakama ya Makadara jijini Nairobi imemhukumu mwanadada mmoja kifungo cha miezi 9 jela kwa kuvunja vikombe na sahani za mama mkwe wake wakati alikuwa mlevi.Mwanadada huyo kwa jina Faith Kemunto mwenye umri wa miaka 24 alikiri makosa yake na kusema kuwa hakukusudiwa kufanya uharibifu huo bali ni ulevi ulimtuma kutekeleza hasara hiyo ya kuvunja vyombo.

Kulingana na hati za mashtaka zilizowasilishwa mbele ya hakimu, Bi. Kemunto alishtakiwa kwa uharibifu usio halali na kwa hiari vibao vya milango, betri ya kompyuta, beseni na sahani zote za thamani ya Sh6450, mali ya Bi. Crucifixa Makunda mnamo Desemba 25, 2022, katika mtaa wa Kamulu ndani ya kaunti ndogo ya Njiru, Nairobi, kinyume na kifungu. 339 ya kanuni ya adhabu.

Kemunto alikiri makosa na kusema kuwa mama wa mpenzi wake hakuwa anampenda ndio maana akachanganya na ulevi na kutekeleza tukio hilo.

Alipokuwa akifanya uharibifu huo,mama mkwe alikuwa ametoka kusindikiza wageni na ndipo walisikia kelele za kuvunjwa kwa vyombo huku Kemunto akiwa amejifungia ndani na kutishia kujiua kwa kujichoma kisu.

Polisi waliitwa wakambembeleza akafungua mlango ambapo walimtia mbaroni akiwa mlevi chakari.

Hakimu alimuamuru kulipa faini ya shilingi elfu 20 la sivyo atumikie kifungu cha miezi 9 nyuma ya nondo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top