Thomasi Mwita Masiaga (28) mkazi wa Kijiji cha Itununu Wilaya ya Serengeti aliyekuwa anatumikia kifungo cha nje cha miezi 6 kwa kumfanyia kosa la kumpiga mke wake amekufa kwa kujinyonga siku aliyotakiwa mahakamani kwa kesi ya talaka.
Amesema,kwa mjibu wa maelezo ya mama yake amewaambia kuwa kutokana na kesi hiyo ya mke wake alikuwa anasema anaweza kujiua maneno ambayo wameamini baada ya kumkuta amekufa kwa kujinyonga.
Masanda Masiaga kaka wa marehemu Thomas ameiambia Serengeti Media Centre kuwa wameshangazwa na uamzi wa mdogo wake kujinyonga ”huyu tarehe 16 alipotoka Mahakamani alikuja na kunieleza mimi na baba mdogo jumatano (18.1.2023) tukamtolee ushahidi wa kesi yake ambayo mke anadai talaka,”amesema.
Amesema,walikubali na walikuwa na maandalizi hayo,na baada ya hapo hakuwashirikisha chochote zaidi ya alfajiri kupigiwa simu kuwa kajinyonga,
”kwanza alikuwa hajamaliza kifungo chake cha nje cha miezi sita alichofungwa kwa kosa la kumpiga mkewe,na kesi hii ambayo mke anaomba talaka ilikuwa inaelekea mwisho na yeye kaamua kajiua,”amesema.
Amekiri kwa muda mrefu kulikuwa na mgogoro baina yao wawili na kifamilia waliwahi kuwasuluhisha bila muafaka na kwa muda mrefu kidogo mke anaishi kwao na watoto,hata kwenye msiba hawajafika.
Kwa mjibu wa taarifa toka Mahakama ya Mwanzo Mugumu kesi hiyo ya Talaka imeahirishwa leo Januari 18 hadi 19,2023 baada ya mdai mke wake jina tunalo kufika na mdaiwa Thomas kutoonekana kwa kuwa hawakuwa na taarifa ya kujinyonga kwake.