Kama unafikiri mwaka 2023 umeuanza vibaya, labda kwa kukosa pesa za matumizi na kuhudumia familia, ama kuandamwa na madeni, basi fikiria upande wa Bibi huyu Mjane, Maua Mohamed, aliyejikuta akiuanza mwaka kwa kulea familia yenye watoto wa tatu, katika maisha ya kutangatanga, baada ya nyumba aliyokuwa akiishi kwa hifadhi kuporomoka.
Maua ameiambia Wasafi Digital kupitia Ripota wetu wa Dar es Salaam @hamisimguta kuwa, awali aliishi kwenye nyumba hiyo iliyopo Ulongoni B, eneo la Mwembe Supu kama wapangaji, lakini baada ya mume wake kufariki, mmiliki wa nyumba hiyo aliamua kumpa msaada wa hifadhi bila kulipa chochote, huku akisalia na maisha magumu yaliyompelekea kufanya kazi ngumu ili apate pesa ya kusaidia watoto wake.
Lakini Ngombe wa Masikini hazai, hatimaye wakati ugumu huo wa maisha ukiendelea kuitesa familia hiyo, Januari 22, mwaka huu 2023 ndipo nusu shari ikageuka kuwa shari kamili, kufuatia kunusurika kufa yeye na familia yake kwa kuangukiwa na nyumba hiyo, na kujikuta wakokosa makazi ya kuishi.
Kwa sasa Maua anaomba watanzania wamsaidie ili apate hifadhi yeye na familia yake sambamba na msaada wa chakula, Ikiwa umeguswa na utahitaji kutoa msaada wowote kwa familia hii, unaweza kuwasiliana na Mtoto wa Bibi Maua (Halfani Omary) kwa namba 0787317121 lakini pia kama unaguswa kuchangia kiasi cha pesa, unaweza kutuma kupitia namba hiyo ya Airtel Money kwa usajili wa jina la Sada Diharibika.
TAZAMA VIDEO HII ITAKUSAIDIA