MTOTO ANUSURIKA KIFO KWA KUNYONGWA KISA KWENDA KWA MAJIRANI

0

 Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka saba mkazi wa mtaa wa Mission, Kata ya Pamba wilayani Nyamagana jijini Mwanza, amenusurika kifo baada ya kunyongwa na shangazi yake Elizabeth Bagwisa kwa madai kuwa alikuwa anacheza nyumba ya jirani ambapo shangazi yake huyo alimkataza.


Majirani wa mtaa huo wamesema mama huyo amekuwa na kawaida ya kumpiga mara kwa mara mtoto pindi anapokosea na kumsababishia majeraha kwenye mwili wake hadi hapo juzi alipoamua kumpiga vibaya na kumnyonga huku akiwa amefungulia redio kwa sauti ya juu ili asisikie mtu yoyote.

Hamisa Juma ni mtoto wa mama huyo anaeleza tukio lilivyokuwa wakati mdogo wake akinyongwa

"Alikuwa amesimama kwenye hii nyumba ya kwanza, alivyomuona amesimama akamuita na kuanza kumpiga Love na mwiko, mama ndiye alikuwa anampiga akampiga sana baadae nikamwambia Love kimbia uende nje akawa anampiga tu hadi baadae akamnyonga," ameeleza mtoto huyo

Musa Fereji mwenyekiti wa mtaa wa Mission anaeleza hatua alizochukua baada ya kupata taarifa za mtoto kunyongwa

"Nilipigiwa simu na wananchi kwamba kuna mama mmoja kwamba alikuwa ananyonga mtoto kweli hicho kitendo kilinishtua sana ikabidi niwatafute wajumbe wangu tukaenda tukamkuta huyo mama akiwa ndani tukamkamata na huyo mtoto kweli alikuwa anaonyesha dalili za kunyongwa maana alikuwa amekabwa shingoni na koromeo,"
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top